Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Raisi Magufuli ameamua ku-deal tu na watumishi wa umma huku akiwapa kisogo wanasiasa wenzake!
Serikali yake imefukuza na kusimamisha watumishi wengi wa umma ndani ya muda mfupi kwa makosa mbalimbali ikiwemo wizi na matumizi mabaya ya madaraka ila mpaka leo hii hakuna mwanasiasa yoyote alieguswa wala kutuhimiwa na hii serikali yake utadhani wanasiasa hawa ni wasafi sana au wao ni malaika!
Kama haitoshi,leo hii anakuja na wazo la kupunguza mishahara ya watumishi wa umma.Sawa ni wazo zuri.Lakini je,katika hali ya kawaida, unawezaje kuongelea swala la kupunguza mishahara ya watumishi wa umma bila kuongelea sitting allowance za wabunge zinazotafuna mabilioni ya walipa kodi wa nchi hii?
Hivi si bora kumlipa "standing allowance" traffic anaeshinda kwenye jua/mnvua akiongoza magari barabarani kuliko huyu mwanasiasa anaekaa kwenye kiyoyozi tena wakati mwingine huku "akisinzia" kufanya kazi ambayo kwa nature ya kazi yenyewe ni lazima akae?
Magufuli kila siku anaongelea swala la kubana matumizi,lakini niambieni ni lini mmemsikia akiongelea hadharani swala hili la sitting allowance za wabunge?
Magufuli ni rafiki mzuri sana wa wanasiasa wenzake lakini ni rafiki wa mashaka sana kwa watumishi wa umma.