Magufuli amekosa exposure

Sawa, sasa tupe njia ya kumsaidia kupata exposure. Je anze safari za nje ya nchi kila wiki, ajipe ubalozi marekani labda Egpyt au aende akasome Edinburgh kama Nyerere.
Atafute nchi ambazo zilikuwa masikini kama sisi miaka ya 60 zikaendelea kama singapore ,malaysia nk ajenge urafiki nazo ,pia kama kuna wazungu wana nia njema na sisiasijifanye masikini jeuri wakae wafanye mikataba ya maana sio ya kilaghai kama ya wenzake (ukimtoa Nyerere)bado ana nafasi,kumbuka mwalimu wakati wa mwanzo wa uhuru alikuwa upande wa mabepari akivaa suti na tai akagundua sera zao hazikuwa rafiki kwetu akahamia kwa wajamaa,(china na urusi )akaanza kuvaa kama Mao.
 
Lengo la hii mada ni kuonesha jinsi JK alivyopanda chopa kwenda Msoga asubuhi na kurudi nayo jioni..
 
Basi walau awe anaangalia CNN, BBC, Al Jazeera etc, walau apate virtual exposure
 
madiplomat wenyewe majipu tuu,sijasema asafiri bali abadili mtazamo wake kwa nchi za kigeni na awe makini na mikataba mipya,asidhani tunaweza kuendelea kutegemea kenya ,uganda na rwanda ,sudan kusini sijui burundi ndio walewale wote tunapambana hakuna wa kumbeba mwenzake
 
Da
kwa kwel kk umenena equal distribution
 
Ushauri mzuri. Japo ningependa nikukumbushe sera ya mambo ya nje bado ipo vilevile kwa hiyo huwezi kusema ana wakimbia wazungu.
 
Kwahyo magufuli akisafiri ndo uchumi utabadilika mkwere aliyekua angani mda mrefu alilisaidia mini taifa. Magufuli anajitahidi kwa kiasi chake Tanzania itaendelezwa na watanzania wenyewe mzungu wala mchina hao wanatu exploit tu ili kujinufaisha. Sioni shida ya kutumbuliwa watu at least heshima imeanza kurudi kwenye sector mbalimbali na accountability japo mapungufu hayaishi.
 
Umesema vema hasa kuhusu Dar es Salaam. Kwa mtu asiye na historia ya kutoka nje ya nchi kwake Dar ndiyo bonge la jiji wakati kiukweli ni "kijiji kikubwa" kuliko vyote duniani tena kisichovutia. Kuhusu kuwakimbia wazungu sidhani kama kuna ukweli wowote. Ninachokiamini ni kwamba Rais kajiwekea mipango yake wakati ukifika na ikiwa kuna jambo la muhimu atatoka tu.
 
Kama ni upeo wa namna hiyo basi tungemchagua wema sepetu,tunataka kiongozi anayejua shida za watanzania siyo muuza sura kama yale jamaa ya ukawa.
 
kwa aina ya uvaaji wake, uzungumzaji wake na hata style yake ya kazi ameanza kwa kufeli time will tell
 
JK noma, duh.

Rais magufuli amekosa exposure ya ulimbukeni. Na nchi haihitaji
 
Ataanza kusafiri kama aliyepita mwisho mje mlalamike hapa.
 
hivi unaweza ukakaa ndani dili zikajileta zenyewe,usidhani rais wa China na Obama kuja TZ mwaka 2013 walikuja kuuza sura,walikuwa wanafukuzia dill,hata wewe ulipomaliza chuo ulisambaza CV kutafuta kazi,ungekaa ndani hata hii simu unayotumia usingenunua
 
kwa aina ya uvaaji wake, uzungumzaji wake na hata style yake ya kazi ameanza kwa kufeli time will tell
Ha ha ha haaah eti uvaaji na uzungumzaji wake....!!!
 
Kuna mambo fulani kama unayakosa, inabidi ukubali tu kuwa huwezi na umuite mwingine mfanye kazi pamoja kwa manufaa ya wote. Sisi tuna rasilimali lakini hatuna teknolojia, so hatuwezi kukomalia tu kwamba wageni wanatunyonya. Mfano, tungewezaje kujua kama tuna gesi ya kumwaga nchini mwetu kama tusingeingia makubaliano ya uwekezaji na watafiti kutoka nje ya nchi? Wao wanayo teknolojia ya kujua wapi pana gesi, wapi pana uranium, wapi pana mafuta etc. So lazima tushirikiane nao, tuwaite waje kuwekeza katika tafiti na uvunaji, then tuingie mikataba iliyo wazi yenye kutunufaisha wananchi wengi. Lakini kama tukisema kila kitu tunaweza (wakati sio kweli), watoto wetu kukosa huduma bora za afya, maji na elimu wakati tunazo rasilimali za kugharamia hayo yote
 
Jamani Ras Simba apelekwe ikulu akasaidie.
 
Ilikuwa bongo movie
pale JK alituweza kweli ila kaiga kwa Godfather wake mzee Ruksa,muda wote yupo pale msasani sijui mikocheni wakati alitakiwa awe kivule au makunduchi zanzibar
 
Nini maana ya ubalozi?

nini maana ya baraza la mawaziri?

nini maana ya makamu wa rais?

JPM tangu aingie madarakani na hajawahi kwenda nje ya nchi, mapato yamepanda au yameshuka(kama mfuatiliaji jibu unalo) Na je angeenda nje ya nchi nani akifuatilia hayo mapato?

Unaijua bajet ya ziara ya Rais nje ya nchi? bajeti ya rais kusafiri nje ya nchi ni tofauti na ya kiongozi yeyote yule wa serikali( Rais anakuwa na msafara mkubwa na weje gharama include security).

Hao wasaidizi wake wanatosha kabisa kumuwakilisha JPM. Hivi unafahamu kwamba Rais ni taasisi? Rais atakuwa wa ajabu kwamba hata kuchukua tuzo aende nje ya nchi wakati kuna mabalozi wake.

Nchi inapoteza heshima yake kutokana na Rais kwenda nje ya nchi pasipokuitwa.. Mimi sitashangaa JPM akialikwa nje ya nchi afu akaenda, maana hapo anakuwa ameitwa yeye hajajipeleka.

Sifa ya Rais kukaa ndani ya nchi na kutatua kero za wananchi.

Unapozungumzia kero ya msongamano wa magari barabarani(foleni) lazima uitaje Dar, itakuwa wa ajabu unaacha kutibu tatizo kubwa unatibu tatizo dogo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…