After daraja kujengwa, najua nauli ya daladala toka kigamboni itakuwa sh. 300, si watalalamika tena ongezeko la nauli!!
Kwa namna moja daraja linaweza kua substitute ya panton, na pia lisiwe hivyo.
Panton unavukia ferry au magogoni karibu na kwa yule mpangaji wetu, so kama unafanya kazi Posta, au unasoma IFM inakua poa tu
But daraja unavukia vijibweni ambapo unakuja kutokea Kurasini eneo linaloitwa "Highway", ambapo mpaka uje uikute Posta itabidi upande daladala za Kariakoo-Shimo la Udongo ushukie Bandari, kisha utafute zingine za Posta kwani hizi hazifiki Posta.
Na kama ni mtu una usafiri wako binafsi, itabidi ukamuliwe mafuta zaidi kutokana na huu mzunguko ulioongezeka mpaka kuingia mjini.
Sasa wakazi wa Kigambini wanapolalamikia ongezeko la Nauli ya Kivuko, hakuna ahueni kwa uwepo wa hili daraja.
Sanasana litawasaidia wenye magari kupunguza foleni siku za wikiend wakitoka Beach.
|
Suala lingine ni kua ni wazi kua kipande cha barabara kutoka "keep-left" cha Bandari pale Kilwa Road inapoanzia mpaka "Keep-left" cha Gerezani ni chembamba mno kuweza kuhimili magari yaliyoko sasa yanayotoka Mbagala, Mtoni, Kurasini, Temeke, n.k, sasa ongezeko la magari ya kutoka Kigamboni ndio yatazidi kuongeza foleni, hivyo ujenzi wa daraja la kigamboni uende sambamba na upanuzi wa kipande hicho kinachopita pale nje ya BP.