MAGUFULI AIKONGA SEKTA YA AFYA
Sekta ya afya ni muhimu na nyeti mno kwakua inagusa kila hatua ya maisha ya mwanadamu.
Kwa kuliona hili Mh. Magufuli ameamua kuja na sera bora ya afya itakayomfanya kila Mtanzania kuwa na uhakika na afya yake hatimaye kumuwezesha kufanya kazi zake vema na kuinua uchumi wa nchi. Haina maana kwamba haya aliyoadhimia kuyafanya Mh. Magufuli hayakuonekana na viongozi waliotangulia, la hasha bali kila kiongozi hutatua tatizo sugu zaidi lililopo kwenye kipindi chake cha utawala.
Msituletee utani.
Wakati huu ndipo mnajua Afya ni muhimu??
Wakati wa Mgomo wa madaktari Serikali si ilisema madaktari wanataka fedha tu na madai yao hayana mantiki?
Si ni Magufuli huyu huyu aliyesema madaktari wanaiba dawa na kupeleka katika maduka yao despite serikali "kununua dawa za kutosha" na kusema atawashughulikia?
-Hivi hospitali zote kuanzia hospitali ya Taifa(MNH) wanaweza kuwa mafaktari wezi hadi zahanati vijijini?
-Vitanda, mipira ya kujikinga, navyo wanaviiba?
-Hivi kama wanaiba kweli, wameshindwa kuwakamata?
-Kama ni kweli wameshindwa kuwakamata kwanini walioshindwa wako kazini hadi sasa?
Tatizo sugu? leo? Usugu upi, madawa, wataalamu wachache, vitendea kazi kukosekana, huduma mbovu au usugu gani unaoungelea?
BIMA? iko wapi mifuko ya bima iliyokuwa ikiwasaidia wananchi mf. Community Health Insurance Fund, CHIF na nyinginezo?
Bima ya afya: Unajua ni dawa ngapi zisizotolewa na mfuko wa bima wa taifa(NHIF) despite mfanyakazi kukatwa kila mwezi?
Afya ya mtanzania imeshachezewa(kuanzia afya ya Akil), hata wao kwenda kutibiwa nje si kwamba wanapenda ila wanajua hali halisi, so msilete porojo hapa.
Tusubiriane tu, Oktoba 25.