DAMAS DAMIAN
Senior Member
- Apr 8, 2011
- 115
- 54
Ni zaidi ya mara tatu mgombea wa CCM anasikika kwenye mikutano akiwataka watu wasifanye mabadiliko kwani yanaweza kutokea mambo kama ya Libya, hii ni dhahiri ya kwamba CCM hawana pakutokea maana wameona kuhubiri ubaguzi kumefeli, kuwatumia viongozi wa upinzani kumefeli na sasa wanawatisha wapiga kura kwa hoja za kitoto, hili nalo linafeli. CCM na Magufuli mnapaswa kujua yafuatayo:-
1. Libya Ghadafi aliingia kwa mtutu wa bunduki na ametolewa kwa mtutu wa bunduki, sisi kwetu tunapiga kura tena kwa amani.
2. Huu sio uchaguzi wa kwanza kufanyika Tanzania na tumekuwa tukipata viongozi kwa amani, mwaka huu kipi cha ajabu?
3. Hatuwezi kufikia walipo libya sababu ya undugu uliopo miongoni mwetu licha ya tofauti za vyama hata ndani ya familia.
4. Ni ujinga kuhubiri kwamba ukipewa ridhaa utafanya mabadiliko ndani ya chama na serikali halafu wakati huo huo unawatisha wananchi wasifanye mabadiliko.
Uhai unapotaka kutoka lazima kutapatapa, mabadiliko mwaka huu ni lazima.
Damas Damian,
Bavicha Korogwe