Magufuli abebeshwa zigo la Zanzibar

Msenyele

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
338
86
Dar es Salaam.Hakuna shaka kwamba mwarobaini wa mgogoro wa Zanzibar kwa kutumia jitihada zandani, sasa ni Rais John Magufuli baada ya jitihada za viongozi wa kisiasa visiwani kukwama, wadau waliozungumza na Mwananchi wameshauri.Mgogoro huo, ambao umekuwa kawaida kuibuka kila baada ya Uchaguzi Mkuu, uliibuka baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha kufuta matokeo Oktoba 28 na kuahidi kuitisha uchaguzi mwingine ndani yasiku 90, kitendo ambacho CUF ilikipinga ikidai kuwa mgombea wake wa urais, Maalim Seif Sharif Hamad alishinda na hakikubali uchaguzi kurudiwa.Tangu wakati huo, Maalim Seif, Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na marais wa zamani wa Zanzibar, Dk Salmin Amour, Ali Hassan Mwinyi na Amani Karume wamekuwa kwenye mazungumzo ambayo mapema wiki hii yamedhihirika kuwa hayajazaa muafaka.Kauli na matukio kadhaa ya hivi karibuni yametoa picha kwamba hakuna maelewano kwenye mazungumzo hayo, huku sherehe zaMaadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi zikiibua mazito zaidi.Akizungumzia kukwama kwa mazungumzo huyo, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), TunduLissu alisema mgogoro wa kisiasa unaoendelea Zanzibar ulikuwa ni wa Kikwete ambaye amemtwisha Rais Magufuli.Mwanasheria huyo mkuu wa Chadema alisema kutokana na hali hiyo, Dk Magufuli ndiye anayeshikiliakete ya utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar kwa kuwa ndiye mwenye sauti ya kusema nini kifanyike.Lissu, ambaye alikuwa akizungumzana Mwananchi kwenye mahojiano maalumu, alisema kutokana na jinsi muundo wa Muungano ulivyo, Tanzania Bara ndiyo yenye uamuzi wa mwisho kwenye mgogoro huo.“Kama Magufuli akisema ZEC watangaze matokeo yatatangazwa mara moja,” alisema Lissu huku akionyesha kusikitishwa na yale yanayoendelea Zanzibar.Lissu alisema Dk Magufuli amerithi mgogoro mkubwa wa Muungano na kisiasa ambao mataifa ya Magharibihayapo upande wake.“Hayakuwahi kuweka msimamo wa wazi wakati wa (Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin) Mkapa na Kikwete, lakini wakati huu yamesema hapana na yameshikilia msimamo,” alisema wakili huyo maarufu nchini.Rais Magufuli ameshakutana na pande zote kwenye mgogoro huo, akianza na Maalim Seif na baadaye Dk Shein. Juzi, Maalim Seif alimnukuu Balozi Idd akisema baadaya mazungumzo na wawili hao, aliwaambia wafuasi wa CCM kuwa Rais ameagiza pande zote mbili zirudi Zanzibar kukubaliana kurudia uchaguzi, kauli ambayo katibu huyo mkuu wa CUF aliikana vikali.Dk Shein ameshaeleza kuwa msimamo wa kurudia uchaguzi wa Zanzibar ni wa chama chake cha CCM na hivyo kuwataka wafuasi wasubiri tarehe itakayotangazwa na ZEC.Kwa sasa, Rais Magufuli ni mjumbe wa kawaida wa vyombo vya juu vya CCM, ambavyo ni Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, lakini anatarajiwa kuachiwa uenyekiti wakati uchaguzi mkuu wa chama hicho utakapofanyika miaka miwili ijayo, au iwapo Kikwete ataamua kuachia mapema wadhifa huo kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake.Kauli ya Lissu ya kumtaka Rais kuingilia kati inalingana na wito alioutoa Maalim Seif juzi jijini Dar es Salaam aliposema ana imani na Dk Magufuli kumaliza tatizo hilo.Seif aliwaambia waandishi wa habari kuwa Dk Magufuli hakuwahi kuwaambia kuwa warudi Zanzibar kukubaliana kurudia uchaguzi, bali wazungumze na kufikia muafaka.Wito wa kutaka Rais Magufuli aingilie kati mgogoro huo, pia imetolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Nicholaus Mgaya akisema heshima ya Dk Magufuli inaweza kusaidia kutatua mgogoro huo.“Naona Rais Magufuli ana nafasi kubwa ya kumaliza mgogoro Zanzibar kwa sababu ni kiongozi anayeheshimika na pande zote mbili zinazotofautiana,” alisema.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema Rais anaweza kutatua mgogoro huo,lakini ni iwapo pande zote mbili zitataka aingilie kati.“Kama wakiendelea hivi kila mtu kushikilia msimamo wake, Rais Magufuli hataweza kutatua,” alisemaBana, ambaye amebobea kwenye sayansi ya siasa. “Wakikaa kwanza na kukubaliana Magufuli awasuluhishe, hapo itakuwa rahisi kuingilia kati na kumaliza mgogoro.”Dk Bana pia alizungumzia ushiriki wa vyama vingine kwenye mazungumzo hayo.“Wanapaswa kutafakari upya. Nadhani ni wakati wa kushirikisha vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi Zanzibar. Vyama hivi vihusishwe kwenye mazungumzo maana CUF wanaweza kususia uchaguzi, lakini vyama vingine vikashiriki. Wanapaswa kukaa kwa pamoja na kukubaliana kama uchaguzi unarudiwa wote washiriki na kama haurudiwi asiwepo hata mmoja atakayekwenda kinyume.”Hadi sasa, pande hizo zimeshafanyavikao vinane ambavyo havijafikia muafaka. Kwa mujibu wa Maalim Seif, CCM wamekuwa wakieleza kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi, lakini hadi sasa wameshindwa kuwasilisha uthibitisho kwenye vikaohivyo.Kauli za wasomi Akizungumzia mkwamo huo, Profesa Mwesiga Baregu alisema wanaojadili muafaka wanapaswa kukumbuka machafuko ya kisasa ya mwaka 2001 yaliyosababisha watu kupoteza maisha.“Mazungumzo yaanze upya kwa kumshirikisha mtu wa tatu. Tunachokiona sasa ni CUF na CCM pekee kukutana. Hawa wanaonekana wameshindwa kufikia muafaka kutokana na kauli wanazozitoa. Tunahitaji uwepo wa watatuzi wa migogoro kutoa nje ya nchi,” alisema Profesa Baregu ambaye amebobea kwenye uhusiano wa kimataifa.“Tanzania imekuwa hodari kwa kutatua matatizo ya nchi jirani. Sasa ni wakati wa kuzishirikisha nchi hizo kumaliza hali ya kisasa inayotishia kuitafuna Zanzibar.” alisema.Kuhusu hilo, Dk Bana alisema tatizo la mgogoro wa Zanzibar ni muundo wa Muungano.“Tungekuwa na muundo wa Muungano wa Serikali moja, tusingeona malumbano kama haya yanayotokea Zanzibar,” alisema.Lakini hakukubaliana na hoja ya Profesa Baregu kuwa mataifa ya nje yashiriki kutafuta muafaka.“Matatizo ya Zanzibar yatamalizwa na Wazanzibari wenyewe. Watu wa nje wanaweza kutoa ushauri tu na rasilimali fedha,” alisema.Alisema ni lazima mazungumzo yafanyike sasa kufikiwa muafaka kwa sababu mgogoro huo una atharikubwa kisiasa, kiuchumi na kijamii.Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim alihoji kama tatizo la Zanzibar ni uchaguzi pekee.“Mpasuko Zanzibar upo muda mrefuna inaonekana hakuna njia muafaka zilizochukuliwa. Je, Zanzibar tatizo ni uchaguzi pekee?” alihoji.Alisema hata ilipoundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bado Zanzibar ilikuwa na tatizo kubwa kwa kuwa wanaoshirikishwa katika mazungumzo hayo ni CCM na CUF pekee, wakati jambo hilo linawahusu Wazanzibari wote.“Mnapotatua migogoro lazima muweke misingi ya makubaliano yenu na lazima mjifunze cha kusema wakati mazungumzo yakiendelea. Si kila mtu kusema lakena kuonekana wazi mnatofautiana.” Alisema taasisi na mashirika yasiyo ya kiserika nayo yana nafasi kubwa ya kumaliza mkwamo huo wa kisiasa.Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo naye alionyesha wasiwasi wake juu ya kauli zinazokinzana za viongozi hao.Alisema siku zote migogoro hutatutiliwa katika meza ya mazungumzo.Mkurugenzi Mtendaji wa Taaisis ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini (Repoa), Profesa Samuel Wangwe alisema kinachoendelea sasa si dalilinzuri kwa amani ya nchi.“Kauli za viongozi wanaotueleza kuwa wapo katika mazungumzo hazileti matumaini ya amani. Nashauri kuanza upya kwa mazungumzo kwa dhamira ya hali ya juu ya kufikia muafaka,” alisema Profesa Wangwe.
 
Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki zanzibar tunaomba muafaka ufikie kwa amani mambo yaishe tuijenge inchi yetu changa kiuchumi
 
Sasa watu wataijua CCM halisi maana wengine ni madekio tu pamoja na JPM. Nina maana hana ubavu wa kuutatua huo mgogoro kwa sababu hana pa kuanzia na nadhani haijui hata katiba ya Zanzibar.CCM ni ile ile
 
mgogoro wa Zanzibar unasababisha na ccm baada ya kushidwa uchaguzi hili lazima liwekwe wazi, na kama ccm watangangania kurudia uchaguzi kurudiwa lazima damu itamwagiga Zanzibar na huku bara pia maana hata sisi wana CUF wa bara hatutakubali itakuwa ni ugomvi na maandamano kama itakavyokuwa Zanzibar ccm wasitegemee kwamba wana CUF wako Zanzibar peke yake,huo utakuwa mziki mkubwa pia waelewe kwamba kuna kitu kinaitwa UKAWA hivyo na wapenzi wa chadema inawahusu
 
Kwa mtu ambaye yuko nje na si Mtanzania ama Mzanzibari in vigumu sana kuelewa kwa nini viongozi wakuu wanashindwa kutoa jawabu la mgogoro huu. Wananchi wa kawaida wa Zanzibar hawajaonyesha dhamira yoyote ya kukataana wala kubaguana. Kampeni ziliendeshwa kistaarabu. Kura zikapigwa kwa Uhuru na haki na hili lilishuhudiwa na observers wa ndani na nje. Kura zikahesabiwa kwa amani kwa maana kwamba hakukuwa na matukio yoyote ya kuzuia kura zisihesabiwe. Matokeo yakaanza kutangazwa. Mwisho yakastishwa na kufutwa! Kwa mtu asiyejua historia ya Zanzibar ataona jambo hili ni la ajabu! Tunaomba viongozi na wahafidhina wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wasiwe 'watumwa' wa historia bali waangalie maslahi mapana ya wananchi na maisha yao kwa ujumla. Msuguano na mgogoro huu unawumiza zaidi wananchi wa kawaida kuliko wao viongozi. Pia inatia doa kubwa muonekano wa Tanzania nchi za nje - Tanzania kwa miaka mingi imekuwa na sifa kubwa ikijulikana kama nchi ya AMANI na imekuwa mfano wa kuigwa.
 
  • Hivi kweli viongozi wa juu wa Zanzibar wameshindwa kutatua na kuumaliza mgogoro huu hadi Rais Magufuli abebeshwe hill zigo? "Mzigo mzito mbebeshe Mnyamwezi"! Rais Magufuli sio 'mnyamwezi'! Watafutwe Wanyamwezi ndani ya Zanzibar maana wamo, wabebe hilo zigo hadi walipatie ufumbuzi na kulitua!!
 
Sio kwamba kabebeshwa zigo, huu ni mzigo wake kuanzia anataka au hataki. Zanzibar ikichafuka bara hakutabaki salama pia. Ikumbukwe yeye ni Rais wa JMT.
 
  • Hivi kweli viongozi wa juu wa Zanzibar wameshindwa kutatua na kuumaliza mgogoro huu hadi Rais Magufuli abebeshwe hill zigo? "Mzigo mzito mbebeshe Mnyamwezi"! Rais Magufuli sio 'mnyamwezi'! Watafutwe Wanyamwezi ndani ya Zanzibar maana wamo, wabebe hilo zigo hadi walipatie ufumbuzi na kulitua!!
mgogoro wa Zanzibar wala sio mzito ni mwepesi sana ila ccm hawataki kuunyanyua tu, mimi nikipewa huo mzigo nitautatua kwa dakika tano tu,maana ni kuwaambia ccm wakubali kura zitangazwe na baadae atagazwe mshindi tabu ya ccm wameshaona kuwa wameshindwa kwa hiyo hata uchaguzi ukirudiwa wakiona wameshindwa hawatakubali, hivyo kumaliza mgogoro ni kumalizia kutangaza matokeo na mshindi atangazwe kwa maana hiyo haiitaji dakika zaidi ya tano kuumaliza mgogoro wa Zanzibar
 
Back
Top Bottom