Magufuli aagana na rafiki yake Odinga

Naona kuna vitoto vinacheza juu ya kibanda hapo nyuma ya mama Janet Magufuli, ni vijukuu vya rais? Vimependezesha picha sana. Halafu inaonekana rais JPM anapenda sana maisha yake ya asili ila majukumu tu ndio yanamfanya abaki mjini.
 
Kwani rais akiwa dar hapumziki? Halafu urais sio kubeba matofari ili kujenga nchi, akiwa popote anaweza kufanya kazi, kama unabisha jaribu kukwepa kodi bandarini uone kama utafanikiwa.

Hapa kazi tu. Magufuli oyeee, chato oyeee, CCM juu. Tanzania Imara.
 

Mwanaume ni kupambana na changamoto. ...ndio maana kwenye maisha kuna watu wanaenziwa mno sababu ya uthubutu wao. Wewe tafuta mteremko tu uone utaishia wapi
 
POPOMA upo dar sio?
 
Yumo humumuhumu nchini na kazi yafanyika kama kawa....
 
Jibu zuri sana la kiuweledi wa hali ya juu.

Tupo Pamoja Sana Mkuu Katika Kuwaelimisha Ambao Kwa Bahati Mbaya Sana Tumewaacha KIUPEO Na KIAKILI. Napenda Mno KUWAAMBUKIZA Watu FIKRA ZA KIMANTIKI Na ZILIZOTUKUKA Ili Ikiwezekana Basi Taifa Letu Liwe La " Majiniasi " Tupu!
 
POPOMA upo dar sio?

POPOMA Shangazi Yako! Sipo Dar Hivi Nyie Mbona Mnalazimisha Mimi Kuishi Dar? Nitafutieni Basi URAIA Wa Huko Kwenu Ili Nihamie Kwani Nimewachoka Sasa. Jamani Mimi Ni MNYARWANDA Kabila La KITUTSI Na Nipo Nchini Kwetu Rwanda Mwaka Wa 11 Huu Ila Niliwahi Kuishi Tanzania Wakati Nikichunga Ng'ombe Zetu Za " Ankole ".
 
View attachment 334691 Rais Magufuli alitembelewa kijijini kwake Chato na rafiki yake kipenzi Raila Odinga kwa takribani siku tatu na leo Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Kenya ameondoka kurejea Kenya.
Hivi huyu Odinga amegongewa Passport? Au ndiyo mambo ya kujuana. Hata kuingia nchini sijui kama maafisa wa Uhamiaji walikuwa makini. Majipu ni mengi!
 
OTE="kijana wa leo, post: 15770216, member: 61737"]Hivi uyo dada nyuma yao ndo yule anayesukaga twende kilioni?[/QUOTE]
Hapana, sio yeye, huyo alikuwa mlinzi wa mama Tunu Pinda.
 
magufuli asipokuwa makini atasababisha mgogoro na rais Uhuru Kenyata...Haya mambo ya urafiki na wapinzani wa serikali sio mazuri kabisa..Kesho Uhuru Kenyata akianzisha urafiki na Maalim Seif itakuwaje
Du!
 
Hawa ni kweli ni marafiki walioshibana angalia hata nguo walizo vaa hadi viatu vinafanana! Mungu azidi kuwa nawe ndoto yako ya kuwa rais itimie tujenge Africa! Huyu Kenyatta ni mswahili sana kama toto la kike
 
Msamehe bure Magufuli ,ingekua ni Jakaya saa hizi yupo zake anabembea kwenye mabembea Jamaica
 
una umri gani..hivi ukiambiwa mtu mwenye madaraka kama ya RAIS, CDF,IGP n.k wapo mapumziko unadhani wana pumzika kama wewe...
 
Tupo Pamoja Sana Mkuu Katika Kuwaelimisha Ambao Kwa Bahati Mbaya Sana Tumewaacha KIUPEO Na KIAKILI. Napenda Mno KUWAAMBUKIZA Watu FIKRA ZA KIMANTIKI Na ZILIZOTUKUKA Ili Ikiwezekana Basi Taifa Letu Liwe La " Majiniasi " Tupu!
naona ume upgrade mwandiko
 
Kumbe ulisoma chuo cha SAUT kilichopo Gisenyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…