dexterous
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 2,037
- 3,134
Saikolojia ni moja ya Sayansi muhimu sana inayohusika na Ufahamu wa binadamu pamoja na akili...
Ubongo wa mwanadamu ni kiungo kiomoja very complex... Ubongo huo huo unaweza ukamuwezesha mtu, kuwa na akili nyingi, na kufanya makubwa, lakini mara kadhaa; kasoro mbalimbali zaweza kujitokeza, na kumfanya mtu kupata magonjwa mbalimbali ya akili/kisaikolojia...
Ifuatayo ni list fupi kati ya magonjwa mengi ya ajabu yanayoweza kujitokeza:
1. Hybristophilia.
Mtu anayesumbuliwa na hali hii, hujikuta tu akivutiwa kimapenzi na wahalifu. Mbaya zaidi watu wa dizaini huu hufika mahali pa kuwasaidia wahalifu hao kama majambazi, kufanya uhalifu...
Halii hii ya kisaikolojia ni common zaidi kwa wanawake kuliko wanaume...
2. Stockholm Syndrome
Hali hii hujitokeza pale mtu aliyetekwa, anavutiwa na hata kumpenda yule mtu aliyemteka. Case ya namna hii pia hujitokeza kwa watu waliongiliwa kwa nguvu kimapenzi na hata kwa watu walioteswa kwa muda mrefu, kufika mahali kuwapenda wanaowatesa, na kuona kama vile wanastahili mateso hayo...
3. Diogenes Syndrome
Hii hutokea zaidi kwa wazee... Ni hali ambayo mtu anakuwa hajijali mwenyewe kiafya na hata kiusafi. mara nyingi watu wa hali hii huishi kwenye mazingira machafu, na hata afya zao huwa mbovu...
4. Cotard's Syndrome
Hii ni hali ambayo sio common sana. Watu wanaosumbuliwa na hali hii, hujidhani kwamba hawapo hai, yaani wameshakufa. Na huishi bila hofu ya kufa, kwani wanaamini tayari wao ni wafu...
5. Synethesia
Hii nayo ni rare case... Humfanya mtu a-feel vitu ambavyo watu wengine hawawezi ku-feel. Kwa mfano: wengine huona ala za muziki kwa macho yao wakati muziki unapokuwa ukipigwa, wengine hudai kwamba wanaweza wakanusa maneno, wengine hudai kwamba kila wakiona maneno; kila herufi huwa na rangi special; jambo linalowasaidia kuwa na kumbukumbu ya muda mrefu...
6. Capgras Delusion
Watu wa namna hii, hudai kwamba mmoja wa rafiki zao au wapendwa wao, amebadilishwa kuwa kiumbe kingine cha kutisha. Na hali hii humfanya mtu kuanza kuwakimbia na kuwaogopa watu hao, kwani wanadhani si watu...
7. Reduplicative Paramnesia
Watu wanaosumbuliwa na hali hii, huweza kufika eneo ambalo hawajawahi kufika kabisa, lakini wakadai kwamba wameshawahi kufika, na kwamba mazingira hayo si mageni kabisa!
8. Munchausen Syndrome
Watu wenye hali hii, hupenda sana kujifanyisha kuwa wagonjwa ili tu wapate special attention kutoka kwa watu wengine. Watu wa dizaini hii pia hufurahi sana pindi wanapoumwa...
9. Apotemnophilia
Hii kwangu mimi ni hali inayotisha, kwani: watu wenye hali hii, hupata hamu/shauku sana ya kukata mguu wake au sehemu nyingine ya mwili wake.
Cha ajabu zaidi, watu wa hali hii, huvutiwa sana na watu wasio na kiungo kimoja au zaidi...
Hali nyingine zaonekana kuchekesha, lakini haya ni baadhi ya maradhi ambayo husumbua sana watu wengine. Dawa ni Tiba ya kisaikolojia tu...