Hili tatizo lilokuwepo hata chuo nilichosoma mimi, Lecturer analazimisha watu kununua vitabu vyake, kuchangia sherehe na hata kuchangia ziara, na anasema kabisa usipochangia tutakutana kwenye course work, kuna Lecturer mmoja alipoona vitabu havinunuliwi akasema atatunga maswali kutoka kwenye hicho kitabu, kitabu chenyewe hata kwenye course outline hakipo na wala hakuna mada inayolingana.
Mimi nilikuwa sina ujinga wa kuchangia michango ya kipuuzi, sijui mambo ya ada ya association ya somo fulani, sikuwa na mpango huo, nakumbuka kuna Lecturer aligoma kunisainia clearance form kwa sababu sikutoa ada ya association ya somo fulani, nikaondoka bila kusaini.
Tatizo kubwa lipo kwa viongozi wa wanafunzi, hata ukipeleka malalamiko kama haya hayafanyiwi kazi, wengi wao ndiyo wanakuwa wahamasishaji wakubwa kwenye mambo ya kuchangisha fedha.