Pishi hili ni maalum kabisa kwa wale ambao ni wageni jikoni au hawajui kupika.Niliomba nipewe pishi la futari ambalo hata asiejua kupika anaweza jaribu na akapatia,nikapewa pishi hili.Shukurani kwa Fetty Kasa
Recipe/pishi la FETTY KASA
Mahitaji
Magimbi
Nazi,tengeneza tui zito na jepesi
Chumvi
Njia
1.Menya na osha vizuri
2. Chemsha na tui jepesi (Tui la pili),yakiiva kabla hayajalainika weka chumvi na tui la kwanza (tui zito).Chemsha adi tui liive na magimbi yawe laini sana.Tui lisikauke,acha liwe rojo jingi.Tayari kwa kula. -ukipenda unaweza weka nyama au mboga mboga zozote.
MziziMkavu hili jimbi ukilipikia na aina supu ya samaki recipe inafanana na ile uloweka basi ndio inaongeza hamu ya kula pembeni uwe na achari ya mbirimbi au ndimu ndo marhabaaaa
MziziMkavu hili jimbi ukilipikia na aina supu ya samaki recipe inafanana na ile uloweka basi ndio inaongeza hamu ya kula pembeni uwe na achari ya mbirimbi au ndimu ndo marhabaaaa