GE2025 Magembe Noni ajitosa Ubunge Jimbo la Geita Mjini

GE2025 Magembe Noni ajitosa Ubunge Jimbo la Geita Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Magembe Noni ambaye ni mzaliwa wa Geita, amechukua rasmi fomu ya kuwania uteuzi wa Chama chake kwa ajili ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Geita Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025

Magembe Noni ni Mtaalamu wa jiolojia mwenye uzoefu mpana katika masuala ya uongozi, usimamizi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kushiriki utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya Serikali kama ni mradi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), pamoja na mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovoti 400 (400kV) unaounganisha gridi ya Taifa ya Tanzania na ile ya Zambia.

Screenshot 2025-07-01 183053.png
 
Back
Top Bottom