Magazeti yanatuchanganya: Makontena mangapi yaliyokamatwa jana?

kivyako

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
14,340
12,049
ce918ce83eb2ea1e98e088c3cbfc8761.jpg
e663e9d8941f4a9812b8eefd30af1856.jpg
fd3ed9d5d6520fe88472ba62e7f8a1d7.jpg
 
Hapo gazeti ni moja tu!! Nipashe! Hayo mengine hayafai hata kufungia maandazi! Kule kwetu tunatawazia n'gombe!! Bora tu niamini figure ya nipashe until otherwise
 
Kwa mujibu wa itv jana saa 2 usiku kichwa cha habari kilikuwa kotena 262 na kiwiliwili cha habari kotena 256.

Lakini kule mchanga huu unapopelekwa uwezo wa kiwanda kuchakata unazungumziwa kwa tani. Akili za kitanzania bado ni tatizo kubwa kwa nini hayo makontena wasiseme yana tani ngapi za huo mchanga? Na thamani yake ni kiasi gani?

Na washawasha!
 
Tuache kuwa Wapumbavu inawezekana!

Tangazo la kuzuia usafirishaji wa Michanga nje ya Nchi lilitoka ghafla Tarehe 3 March, 2017 likielekeza kuwa zuio Hilo limeanza Tarehe 2 March!!

Tangazo halikuelekeza Makontena yaliyoko Tayari Bandarini kwa Safari na Yale yaliyoko njiani ( on transit) yafanyiwe utaratibu upi?

Utaratibu huu wa kijinga unafanana na wa Marufuku ya Viroba halafu unavamia store ya Mfanyabiashara unasema umekamata Viroba wakati hamkutoa Maelekezo ya wapi vipelekwe viroba ambavyo tayari vilikuwa sokoni

Tunazuia usafirishaji wa Michanga nje ya Nchi ili tuchambue Mchanga wetu ndani ya Nchi bila ya ku assess uwezo wetu.

Rais karopokea Mtwara hiyo kauli bila ya kushirikisha Wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini wala Baraza la Mawaziri ndio sababu karopokea Kwmy Mkutano wa Hadhara na bila ya kuwapa Notice wahusika na Matokeo yake Wizara ilitoa tangazo Tarehe 3 na kusema katazo limeanza Jana yake!

Rais hakupatathimini Madhara ya kimkataba kwa Wawekezaji kwa kuanza kuzuia usafirishaji bila ya kujua mambo yaliyokubaliwa kwny Mikataba yana taratibu zake kwny kufanya amendment .

Kiwanda cha kuchambulia Mchanga wa Madini sio Kama kiwanda cha kukamulia Juice ya Miwa.

Economically Huwezi kununua Machine ya kusagia Mahindi kwa ajili ya kusagia Debe zako Tatu za Mahindi kwa Mwaka kwa kuwa Mashineni huwa wanakuibia kiasi cha Unga baada ya kusaga!

Mugabe alipaoanza kupora Mashamba ya Wawekezaji Jumuia za Kimataifa zilimbana na sasa Zimbabwe ni kaburi la Kiuchumi Sadec

Sie tunaelekea Zimbabwe kwa kasi sana
 
Wata wadanganya wachache wasio jua maigizo ya nchi hii.wanagombania kiki za kwenye magazeti mkuu anataka ukurasa wa kwanza atokee yeye na serikali yake janja janja hamna kitu hapo changa la macho
 
Eti huo ndo uzalendo kuweka front page habari zake. Suala la kuhatarisha amani ya nchi watu kuvamia vituo vya redio na silaha,askari kutoa bastola hadharani kutishia watu sio uzalendo. Infact hizo contena sio sindano zimefuata taratibu mpaka zikafika hapo Leo hii mnatuwekea maigizo kua mmezikamata utafikiri zilifichwa mafichoni
 
Kila gazeti Lina idadi yake ya kontena sijui zilikamatwa marangapi ila kwa akili yangu ya kiki naona tuhesabu 260+262+256=778
 
Kila gazeti Lina idadi yake ya kontena sijui zilikamatwa marangapi ila kwa akili yangu ya kiki naona tuhesabu 260+262+256=778
Tuma jina lako tukuweke kwenye shortlist ya kuteuliwa maana umepaisha namba iliyokamatwa mpaka 778! Safi sana huo ndo uzalendo! hahahaha
 
Back
Top Bottom