Magazeti ya udaku yafungiwe

D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
3,160
3,259
Wakuu heshima kwenu

Leo nimejikuta natafakari sana dhamira ya magazeti yanayoitwa ya udaku au kama yanavyojiita eti magazeti pendwa
-kiu
-sani
-ijumaa
-filamu
-uwazi
-risasi.
Kwa ujumla magazeti haya yanaonyesha pasi na shaka kuwa yametawaliwa na waandishi uchwara tena Wasio na taaluma ya uandishi wa HABARI.
Ukijaribu kutafakari kuhusu hayo yanayoandikwa na magazeti hayo mara nyingi
-hukumbusha na kutonesha vidonda vya wafiwa kwani mara nyingi huchapisha habari ili wauze na sio kuangalia HABARI hiyo itapokelewa vipi na jamii.
-hulenga kumchafua mtu,mara nyingi magazeti haya huandika kuhusu mambo ya faragha kumhusu mtu badala ya kuandika mambo ya kuelimisha na kufundisha jamii.
-chuki na husda katika jamii hili utaligundua kwani tukio anaweza kufanya mtu mmoja mfano mwalimu lakini wao hawawzi kusema mwalimu wataandika waalimu
-kupandikiza hofu


Hivyo kwa kuhitimisha mtazamo wangu ni kuwa serikali badala ya kulenga kuyafungia magazeti yanayoikosoa pekee yangefungia magazeti haya yanayoandika kwa minajili ya kuuza pekee badala ya kuhabarisha na kufundisha

Tafakari njema greater thinkers




 
Unataka yule mfadhili Mafisienu , Bw Shigongo afe na njaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…