NADHANI SISI WOTE HUMU TUSIJIDAI TUNAIJUA NATO KULIKO RUSSIA INAVYOIJUA NA PIA TUSIJIDAI KUIJUA RUSSIA KUILIKO NATO WANAVYOIJUA.
Pia mjue tu kua ikitokea vita baina ya NATO Vs Russia kati ya changamoto mojawapo itakayotokea ni Dunia hii kurudi maisha yale ya miaka ya 1945 kurudi nyuma MAANA MIFUMO YOTE YA MAWASILIANO(Satellite) inaweza kuharibiwa . Ndio maana mara nyingi Marekani amekuwa akiituhumu Russia kuhusu mipango yake ya kuzihujumu Satellite zake.
1. Tutarudi enzi za kuandikiana barua
2. Tutarudi enzi za kuizunguka radio kupata taarifa
3. No TV live coverage
4. Ujuaji wa humu Jf hautakuwepo badala yake tutauhamishia kwenye vijiwe vya kahawa na shoe shiners.
Ninachoamini mimi ni kwamba Marekani na washirika wake wakiungana wanaweza kuipiga Russia na kuiangusha LAKINI WANAJUA CHANGAMOTO AMBAZO NCHI ZAO PAMOJA NA DUNIA ZITAPITIA TENA KWA MUDA MREFU SANA.
Pia tujiulize ni kwanini Russia badala ya kusimamisha vita yeye kila siku anasonga mbele na kuchukua ardhi ya Ukraine. HII JEURI NA KIBURI ANAKITOA WAPI???