Magaidi wauwa Watu 28 nchini Somalia

Magaidi wauwa Watu 28 nchini Somalia

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,566
Reaction score
4,013
Walipuaji wa kujitoa mhanga wameuwa watu 28 wakiwemo wapiganaji 6, katika mashambulizi matatu ya mabomu ya kutegwa kwenye magari, mjini Mogadishu, Somalia.

Kundi la wapiganaji la Al-shabaab lenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda, limedai kuhusika na mashambilizi matatu karibu na hoteli ya Sahafi, iliyo karibu na makao makuu ya ujasusi CID.

Maafisa wa polisi wanasema kwamba walinzi wa hoteli ya Sahafi, waliwafyatulia risasi wahanga baada ya mlipuko na kuuawa wapiganaji wanne waliojaribu kuingia hotelini.

Dakika 20 baadaye, mlipuko wa tatu ukatokea karibu na hoteli hiyo kutokana na bomu lililokuwa limetegwa gwenye gari la miguu mitatu maarufu kama Tuk tuk.

Mumiliki wa hoteli ya Shafi, alichukua usimamizi wa hoteli baada ya babake kuuawa katika shambulizi la wapiganaji mwaka 2015, naye ameuawa katika mashambulizi hayo ya leo ijumaa.View attachment 928431
IMG_20181110_094219.jpeg
 
Hawa jamaa sijui kwann hawajifunzi kwa ndugu zao wa somaliland… kule kumetulia hakuna huu ujinga ujinga…
 
Watumishi waaminifu wa Shetani kazini; wakitenda sawa sawa na mapenzi ya baba yao maana kazi zake zi dhahiri; faraka, husuda, chuki, mauwaji, kumwaga damu, na yafananayo na hayo huku wakijidai "kumlingania" yeye aliye muumba.
 
Somaliland ni nchi halisi ya kiislam ingawa umoja wa mataifa umegoma kuitambua ila ukaitambua Sudan Kusini ambayo hawajui maana ya imani.
 
Naelewa unachomaanisha, karibu sana Somaliland ingawa UN imegoma kuitambua kama nchi huru.
 
Somaliland ni nchi halisi ya kiislam ingawa umoja wa mataifa umegoma kuitambua ila ukaitambua Sudan Kusini ambayo hawajui maana ya imani.
Sasa dini zinahusiana vipi hapa mkulu? Nao hao Sudan kusini hawajui maana ya Iman ipi? Kuanzia miaka ya 2000 mpaka sasa nchi zenye kujua “maana ya imani” kama afghanistani.. Yemen.. Syria.. Iraq… Pakistan… imekuwa shaghalabaghala tu… hivi juzi juzi tumeona Saudia na qatar [emoji1203] wakiwavurumishia ndugu zao wa Yemen migruneti na mikimbora ya haja…. Bado unaamini kuwa “Imani” ndo kila kitu?
 
Sorry nlikuwa nataka kusema amani na sio imani. But all in all bado ujumbe uko pale pale hata ningelisema ni imani, Hao iliowataja hawana tofauti na Somalia. Najua haujapendezwa kuona kuna nchi ya Kiislam yenye Amani maana mlishajazwa kasumba kuwa waislam ni watu vurugu tupu. Karibu Darussalam uje ujifunze tofauti kati ya dini na imani.BWANA ASIFIWE.
 
Kwann nisipendezwe na binadamu wenzangu kuwa na amani Mkuu? Kuna Imani zinafundisha wafuasi wao wafurahie mahangaiko ya wengine?
Binafsi niliona kama ni mgogoro wa Somalia sikuwa na dimension ya Iman ila wewe ndo uliingiza Uislam ndo nikataka ufafanuzi zaidi.. Sio kila kitu kina dimension ya dini.. Ingekuwa hivyo basi jamii zenye imani moja (mathalani Afghanistan ama Yemen) tusingekuwa tunasikia chokochoko
 
Back
Top Bottom