kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,154
Kituo cha Kiislamu cha mji wa Bielefeld nchini Ujerumani kimechomwa moto ikiwa ni kuendelezwa chuki za kidini dhidi ya Waislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa Pars Today tukio hilo limetokea mapema leo Jumatano kwenye kituo cha Kiislamu cha Wabosnia na inaaminika kuwa, mtu mmoja mwenye chuki za kidini amekichoma moto kwa makusudi kituo hicho.
Ripoti zinasema kuwa, mshambuliaji huyo ameingia ndani ya kituo hicho na kukichoma moto. Hata hivyo maafisa wa idara ya zimamoto ya Ujerumani wanmeema, kuna uwezekano kitu kimoja kimerushwa ndani ya kituo hicho kupitia dirishani na baadaye kuwaka moto.
Maafisa wa zimamoto walifika mara moja kwenye eneo la tukio kwa ajili ya kuwaokoa wahanga wowote ambao huenda walikuwemo ndani ya kituo hicho.
Michael Graf, mkuu wa idara ya zimamoto ya eneo hilo amesema, maafisa wa idara hiyo walipofika kwenye eneo la tukio waliona miale ya moto katika dirisha lililovunjwa ikitokea ndani ya kituo hicho. Wanasema walimpata Imam wa Sala ya Jamaa ya kituo hicho akiwa kwenye chumba cha chini ya ardhi.
Moto huo umezimwa haraka na watu wote wameondolewa kwenye jengo hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mashambulizi dhidi ya Waislamu na maeneo yao ya ibada na ya shughuli zao mbalimbali, yameongezeka sana katika siku za hivi karibuni huko Ujerumani.
Genge lenye chuki za kidini lijulikanalo kwa jina la PEGIDA limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Waislamu nchini Ujerumani.
Source; Irib