Magaidi wa Boko Haram wanashindwa Nigeria

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
236
306
Kwa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari mambo sasa yanaelekea kuwa mazuri. Yuko katika furaha.

Kabla ya Krismasi iliyopita alitangaza kwamba Jeshi la nchi yake limewashinda wapiganaji wa kundi la magaidi wa Boko Haram. Hapo kabla Jeshi la Nigeria pia lilitangaza kwamba limeliteka eneo la mwisho la maficho ya wanamgambo wa siasa kali za Kiislamu wa Boko Haram katika eneo linaloitwa Camp Zero katika Msitu wa Sambisa.

Ilitajwa kwamba Buhari mwenyewe amejivunia kuhusu majeshi ya nchi yake. Sasa juhudi zaidi zinaelekezwa kuwatafuta watoto wa kike 218 wa shule kati ya 276 waliotekwa nyara na Boko HaramTatizo ni kwamba mwaka mmoja uliopita Buhari aliwahi pia kutangaza kwamba wapiganaji wa Boko Haram “wameshindwa kimbinu.Wakati huo, mwaka 2015 kama ilivyo sasa, mashambulio mengi yalielekezwa kwa Boko Haram.

Kwa hivyo, kundi hilo la kigaidi likawa halina tena nguvu lililokuwa nazo miaka miwili kabla, kabla ya Buhari kuingia madarakani kama rais.Mwanzoni mwa mwaka 2015 wanamgambo wa Boko Haram waliyadhibiti maeneo kadhaa ya Kaskazini Mashariki ya Mkoa wa Borno na maeneo mengi ya mkoa huo yalikuwa hayapitiki. Kurejea kwa Msitu wa Sambisa ulioko milimani karibu na mpaka na Cameroon mikononi mwa majeshi ya Serikali kulionekana zamani kuwa ni jambo muhimu katika kuwashinda magaidi hao.Sasa wapiganaji hao wanaelekea zaidi Ziwa Chad katika mpaka na nchi jirani ya Niger.
 
Mimi huwa naona kama kama maigizo tu ina maana jeshi la Nigeria halijui kabisa kambi ya boko haram?
 
Back
Top Bottom