Mafuta ya taa yameanza kusambazwa kwenye uhaba


K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Likes
1,064
Points
280
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 1,064 280
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa ufafanuzi kuhusu uhaba wa mafuta ya taa na kueleza kuwa mafuta hayo yameanza kusambazwa kwenye maeneo mbalimbali ambayo yana uhaba.

Aidha, imesema inakusanya maoni ya wadau ili kutoa fursa kwa kampuni za Tanzania kushiriki kupata zabuni kwa ajili ya kuleta mafuta nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam kwenye mkutano na wadau wake wa kukusanya maoni, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema maeneo ya Mtwara, Songea na Ruvuma ambako kumekuwa na uhaba wa mafuta ya taa, magari yameshapeleka mafuta hayo.

Ngamlagosi aliwatoa hofu wananchi kwamba nchi haitaingia katika uhaba wa mafuta ya taa kwa kuwa kuna mafuta ya kutosha yanayokidhi mahitaji mbalimbali kwa muda wa siku 16.

“Mafuta yameshaanza kusambazwa katika maeneo mbalimbali nchini ambayo yalikuwa na uhaba wa mafuta. Mafuta yaliyopo yanatosheleza kwa mahitaji ikiwemo mafuta ya ndege ambayo yanatosha kwa siku 30, mafuta ya petroli kwa siku 12, dizeli kwa siku 15, viwanda siku 39 na migodi kwa siku 13,’’ alisema Ngamlagosi.

Akizungumzia chanzo cha uhaba wa mafuta ya taa, Ngamlagosi alisema chanzo cha upungufu huo ni kutokana na meli iliyobeba mafuta ya petroli na ya ndege kuchanganyika hivyo kusababisha kuchafuka kwa matangi na mabomba yote.

Alisema usafishaji wa matangi hayo umekamilika na kwamba mafuta ya ndege pamoja na ya taa hupokelewa kama kawaida, hivyo maeneo yenye uhaba yameanza kufikiwa.

Katika hatua nyingine, Ngamlagosi alisema kampuni nyingi za Tanzania zimekuwa zikishindwa katika zabuni mbalimbali zinazotolewa hivyo kampuni za nje kushinda zabuni.

Alisema wameweka mkakati kuboresha ushindani kwa kuhakikisha kuwa kila meli inayoingiza mafuta nchini inakuwa na zabuni. Alifafanua kuwa jambo hilo litakuwa na faida kwa kampuni nyingi za Tanzania kushiriki kibiashara kuleta mafuta.

‘’Tumeona kuwa kampuni za nje zinaposhinda zabuni Tanzania hainufaiki kutoza tozo ya aina yoyote na badala yake faida inabaki kwao. Lakini Watanzania wakipata zabuni hizi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaweza kukusanya mapato yake na watanzania wengi zaidi watafaidika,’’ alisema Ngamlagosi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kwimba, Mansoor Hirani (CCM) ambaye pia ni mdau wa sekta ya mafuta alisema mapendekezo yaliyoletwa na Ewura yamecheleweshwa kwa kuwa Tanzania imekuwa haipati faida kutoka kampuni za nje.

Hirani alisema kwa miaka mingi kampuni za nje ya nchi ndio wamekuwa wakishinda zabuni zinazotolewa na Ewura. ‘’Kampuni za ndani zina uwezo wa kutosha kusaidia suala la uletaji wa mafuta nchini pia itatoa mwanya kwa watanzania kujiendesha wenyewe,’’ alisema Hirani.

Habari Leo
 
D

DNR

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2013
Messages
524
Likes
318
Points
80
D

DNR

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2013
524 318 80
Kumbe kuna uhaba wa Mafuta ?


kweli ni vigumu kujua sababu watumiaji wengi wako vijijini Tofauti na sukari mjini .
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
1,046
Likes
1,392
Points
280
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
1,046 1,392 280
Kumbe kuna uhaba wa Mafuta ?


kweli ni vigumu kujua sababu watumiaji wengi wako vijijini Tofauti na sukari mjini .
Inakera zaidi wanapsema kuna uhaba Sngea na Mtwara wakati hata Dar es salaam baadhi ya maeneo kuna uhaba wa mafuta ya taa kwa zaidi ya mwezi sasa! Ukikuta mafuta basi lita moja ni Sh. 3000/=.... hili sio la kusikia bali nime-experience mimi mwenyewe na hata hiyo bei ya Sh3000 nimelipa juzi Jumapili!
 
nankumene

nankumene

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2015
Messages
5,556
Likes
5,059
Points
280
nankumene

nankumene

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2015
5,556 5,059 280
Walipoulizwa mara ya kwanza walisema hamna uhaba labda magar yatakua yamechelewa kufika kwe hio mikoa...hawa watu wasahaulifu sana
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
1,046
Likes
1,392
Points
280
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
1,046 1,392 280
Walipoulizwa mara ya kwanza walisema hamna uhaba labda magar yatakua yamechelewa kufika kwe hio mikoa...hawa watu wasahaulifu sana
Wapuuzi tu hao!!! Ina maana hayo magari yamechelewa kufika hata Temeke wakati Temeke ndo kuna matank ya hayo mafuta!!!
 

Forum statistics

Threads 1,237,367
Members 475,533
Posts 29,286,076