Nashangaa wanaosema watu hawatumii mafuta ya taa. Hata mimi nina majilo mengi ukitak hata video natuma
1. Jiko la mchina - Hili hutumika sana kupikia vitu vya mda mrefu kwa sababu nina familia ndogo vinaiva fasta mfano uji wa ulezi, nyama, maharage, kande nk
Huwa nanunua dumu kita 20
2. Jiko la Gas - Hili huwa linatumika sana kuunga mboga za majani, kupika mayai, chai, kukaanga nyama nk
Nanunua mtungi oryx kg 15
3. Jiko la Mkaa - Huwa nalitumia kupika wali na pilau endapo umeme hakuna. Huwa nanunua mkaa gunia
4. Rice cooker - Natumia rice cooker kupika wali na pilau tu
Linatumia umeme
5. Pressure cooker- Mara nyingi hili linatumiwa kwa kupika sana sana supu na viazi roast
Linatumia umeme
6. Jagi za kuchemsha maji - Haya yapo mawili moja la kuchemsha maji ya kuogea. Sikutaka kuweka heater nyumba ina vifaa vingi vya umeme very dangerous. Yapo matatu ila moja ndio la lita 25 kwa ajili ya kuchemsha maji ya kunywa
7. Jiko koa - Hili huwa linatumika nadra sana kupikia lipo lipo tu
8. Convention oven - Kazi yake ni kuchoma nyama, viazi, mihogo na ndizi
Hutumia umeme
9. Slow cooker - Hii inatumika kupashia chakula moto na kuipa mboga taste aisee ukiweka mchuzi humu kwenye slow cooker nyama zinalaika vizuri na zinataste vizuri
Sina: Oven + microwave + induction cooker, planning to buy in the future
Kufupisha jiko la mchina ndio jiko linalotumika sana tena hususani vyakula vya kukaanga kaanga kama ndizi za mzuzu, nyama za kukaanga nk. Kwa hiyo kusema kuwa hayatumiki ni nyinyi ambao hamtumii ila kwa sisi huwa tunayatumia bado. .
La ziada: Gharama huwa nafuu sana ukiwa na majiko tofauti kwa mapishi tofauti tofauti. .