Mafuta nishati yanaendelea kushuka bei

Mafuta nishati yanaendelea kushuka bei

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,014
Reaction score
6,832
DODOMA: WATUMIAJI wa bidhaa za mafuta ya petroli nchini wameuanza mwaka mpya wa 2025 kwa shangwe ya kuendelea kupata unafuu bei za bidhaa hizo kwa mwezi Januari 2025.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeonesha bei za mafuta kuendelea kushuka katika kipindi hiki ambapo petroli kwa lita imeshuka kwa shilingi 105, dizeli kwa shilingi 135 na mafuta ya taa bei imepungua kwa shilingi 15 kwa mafuta yaliyopokelewa Bandari ya Dar es Salaam ikilinganishwa na bei za Mwezi Desemba 2024.

Kwa upande wa mafuta yaliyopokelewa Bandari ya Tanga, bei ya petroli pia imeshuka kwa shilingi 105 kwa lita, dizeli shilingi 136 na mafuta ya taa shilingi 135 huku Bandari ya Mtwara bei ya petroli kwa lita ikipungua kwa shilingi 42, dizeli shilingi 129 na mafuta ya taa shilingi 157.

Ahueni hiyo inatokakana na kuendelea kuimarika thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta nje ya nchi ambapo wastani wa kubadilisha fedha za kigeni umepungua kwa asilimia 11.27.

Ikumbukwe pia kwamba, bei za bidhaa za mafuta aina ya petroli zimeendelea kushuka mfululizo kwa takribani miezi mitano kuanzia mwezi Septemba 2024.

Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
#HabarileoUPDATES
 
Safi
 
Diesel tunazidi kupeta tu. Hadi chuma ifike 2,000/=
 
Hii biashara ya mafuta ni pasua kichwa balaa. Imagine mtu kananunua mafuta tarehe 30 December kwa bei ya juu na possibly hayajafika kituoni mpaka sasa lakini atayauza kwa bei ya chini kutokana na bei za leo.
Kila siku najiuliza kwa nini mafuta yanabadilika bei kila mwezi? Kwani hatuwezi kuwa na constant price hata kwa miezi mitatu consecutively?
 
Hawawezi pata hasara maana mzigo unaouzwa uko reserve kwa kipindi cha miezi miwili sokoni, mogul wa biashara lazima wakae vizuri na idara husika,
Soko la dunia pia mzigo umeshuka bei
 
Back
Top Bottom