Mafuriko yasomba magunia 400 ya mahindi na mifugo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,923
10,457
Zaidi ya magunia 369 ya mahindi na kondoo watano, yamesombwa na maji katika vijiji vya Magasa na Mrijo Juu kata ya Mrijo wilaya mpya ya Chemba mkoani Dodoma, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana.

Mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali imebomoa nyumba tano na kusomba kuku 59 na kusababisha watu zaidi ya 60 kukosa chakula na makazi.

Diwani wa kata ya Mrijo Chini, Hamisi Musakati alisema kuwa mvua hiyo ilikuwa kubwa na kusababisha maji mengi kuingia katika nyumba za wakazi wa vijiji hivyo na kuleta madhara makubwa.

"Kufuatia tukio hilo, familia hizo zimehifadhiwa katika ghala la kuhifadhia chakula la kijiji cha Olboloti zikisubiri msaada wa serikali ngazi ya kata na wilaya," alisema.

Msakati alisema serikali imewahadharisha wananchi waliyopo maeneo yasiyokuwa salama kuhama kwa muda kwani kuna kila dalili kuwa mvua za aina hiyo zitanyesha tena.

Naye mtendaji wa kijiji cha Oloboloti, Bashiri Mtoro, akizungumzia janga hilo alisema kuwa hasara iliyopatikana na mafuriko hayo ni zaidi ya Sh. milioni 200 na hakuna kitu kilichookolewa.

Alisema baadhi ya wananchi hao wamesaidiwa chakula, magodoro na mashuka kwa ajili ya kujifunika hasa kipindi hiki cha baridi kali inayoambatana na mvua za mfululizo mchana na usiku.

Mtoro alisema tukio hilo linawaongezea mzigo hasa ikizingatiwa hivi karibuni kata yake ililazimika kupokea 'wakimbizi' 250 waliokimbia mapigano ya wafugaji na wakulima kutoka wilaya ya Kiteto.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom