Mafuriko Jijini Mwanza

nyakonga

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
200
78
Kuna hali ya taharuki hapa Mabatini kwani kuna mafuriko makubwa hadi barabara ya kutoka Musoma kuingia mjini imefungwa karibu masaa matatu, hakuna gari kupita maji yameenea eneo lote la mabatini (mto Mirongo).

Kwa kweli hili eneo la mto Mirongo panahitaji bomoa bomoa kubwa ili kunusuru wanajiji.
 
Ah, poleni sana ndugu zetu.

Ni jukumu la waliopewa dhamana ya usimamizi wa usafi, mazingira na mipango miji kuhakikisha watu wanaishi maeneo yasiyo hatarishi. Aidha wanapashwa kuhakikisha usafi ni endelevu huku mifereji yote ya maji ikiwa misafi usiku na mchana na ikifanya kazi kama ivyotakiwa. Mwanza hapo ni karibu sana na ziwa na hivyo mara nyingi kumekuwa na hatari kwa binadamu zitokanazo na mvua pamoja na miundo mbinu mibovu ama michafu.

Ujenzi wa holela ni tatizo kubwa sana linapashwa kuangaliwa. Viwanja vipimwe kufuatana na ramani ya jiji ili wanaojenga waonyeshwe maeneo na sheria za ujenzi wa maeneo husika . Kusubiri wamejenga halafu wanapelekewa maji, umeme, soko, na kodi za majengo zinachukuliwa na serikali, na zaidi ya hapo wapimmiwe na kupewa hati za maeneo waliojijengea kiholela kwa malipo ya fedha, halafu siku ya mwihso wanaambiwa bomoeni mmejenga visivyo n.k, ni unyanyasaji wa binadamu, ufedhuli na uzembe unaotakiwa kuiwajibisha srikali kwa kushindwa kazi.

Tuna budget ya mishahara ya kila mwezi ya idara za mipango miji na upimaji na ramani. Wanalipwa kwa sababu ya kuvunja majengo? Wanalipwa kwa sababu ya kuwatoza watu fedha ili wakawapimie maeneo holela? Wanalipwa ili wakei ofisini wasubiri matatizo?

Serikali ya hivi haitupeleki popote. We need to be pro-active and accountable for final results of whatever is under our custody!. Asiyeweza kwa sababu hataki ama kazoea ama kwa sababu yoyote, aondolewe wapewe vijana wanaomaliza vyuo na kazi hawana. Kwanza hawa ni rahisi hata kuwajengea working culture mpya yenye mantiki sahihi ya ajira kwa maendeleo ya umma, umma ambao hata wao wako ndani yake!.
 
Mwanza inasikitisha sana mvua kubwa ikinyesha,njia ya mto milongo iangaliwe kwa jicho la tatu maana ni hatari kwa wanafunzi wadogo
 
Mwanza inasikitisha sana mvua kubwa ikinyesha,njia ya mto milongo iangaliwe kwa jicho la tatu maana ni hatari kwa wanafunzi wadogo
Hivi hakuna namna ya kuyapunguzia kasi maji yanayotiririka kufurikisha huyo mto kila zikinyesha mvua kubwa?
 
Mwanza inasikitisha sana mvua kubwa ikinyesha,njia ya mto milongo iangaliwe kwa jicho la tatu maana ni hatari kwa wanafunzi wadogo
kinachonichosa madaraja. Kwakweli ni hatari sana kwa watoto kupita hasa kipindi hiki cha mvua. Nenda soko la mabatini uone vile vidaraja, nenda daraja la wamasai. HATARI TUPU
 
Back
Top Bottom