Mafuriko Dar es Salaam na Miaka 50 ya Uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuriko Dar es Salaam na Miaka 50 ya Uhuru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kardo Joseph, Dec 28, 2011.

 1. Kardo Joseph

  Kardo Joseph New Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zanguni napenda kutoa masikitiko yangu kwa wapendwa wetu wote waliokumbwa na maafa ya mafuriko jijini Dar es Salaam na pahala pengine popote pale ndani ya nchi yetu. Pia niwape pole ndugu na jamaa ambao wamepotelewa ndugu, mali na kukosa mahala pa kuishi kufuatia maafa hayo. Kuna mambo makubwa matatu ya kujiuliza;


  1. Nini kazi kubwa ya kitengo cha Maafa kilichopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu? Pia kuna tatizo gani kwa watanzania wenzetu kutosikia pale serikali inapowaasa kutorudi tena mabondeni na kuishi huko, wataalam naomba tufanye utafiti wa kina kuona tatizo la kukaidi amri za serikali linasababishwa na nini?
  2. Juzi tumeadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika tena kwa kualika wageni wengi toka nje na ndani ya nchi yetu na kwa gharama kubwa ya kuhodhi ugeni ule, tukaona mambo mengi uwanjani ambayo nchi yetu inayo hususani katika ulinzi na usalama, kukawepo ndege za kivita, askari maji walio mahili na fani hiyo na mambo mengi kadha wa kadha. Je ni kwa kiasi gani jeshi limeshiriki kuokoa wahanga wa mafuriko ya Dar es Salaam pamoja na uwepo wa vifaa na askari walioonekana uwanjani siku ya sherehe za uhuru, mbona hawakuwa mstari wa mbele kuogelea ama kutumia ndege zao kuokoa maisha ya watanzania wenzetu waliopatwa na maafa?
  3. Kitengo cha ardhi ambacho kina wataalam wazuri kabisa wanaotambua mikondo ya maji na ubora wa ardhi kwa makzai ama kwa shughuli tofauti na makazi wanafanya nini mpaka wanawapa ardhi watanzania wajenge maeneo ambayo mkondo wa maji unapita? Pia kuna haja ya kuona uwezekano wa kuboresha miundo mbinu yetu na hususani kubadilisha madaraja yetu barabarani angalau yote yafanane na daraja lile la Ruvu.
   
Loading...