sulai
Member
- Jan 11, 2017
- 58
- 32
Hivi kwanini Serikali huwa wanapotezea sana askari mgambo katika upatikanaji wa ajira serikalini?
Unakuta kijana amefanya mafunzo ya mgambo tena kwa uzalendo wake kabisa lakini ajira zinapotoka za vyombo vya ulinzi wanawapatia vijana wa JKT tu lakini waliopitia mafunzo ya mgambo huwa hata hawawaomei huruma kwamba nao hawa ni vijana wa kitanzania na ni wazalendo lakini hawapatiwi ajira kama zinapotokea hadi labda kwa amri ya amiri jeshi mkuu (Rais).
Sasa huwa najiuliza kuna umuhimu gani wa kuendelea kutoa mafunzo hayo wakati ajira zinapendelea upande mmoja tu? Je, hili suala Chief wa Mgambo huwa halioni?
Kuna vijana wengi waliopitia mgambo na wana sifa nzuri umri sahihi wa kupata ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama lakini wanawapotezea tu, hebu tunaomba Serikali itukumbuke na sisi wanamgambo pia tuna mchango pia katika taifa hili japo huwa hatusikilizwi na wakati mwingine huwa hata kombati zenyewe huwa tunajinunulia sijui ni kwanini