Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Wakati mafunzo yakiendelea maeneo mbali mbali nchini, nami leo naendelea kujadili yale ambayo natarajia yamo kwenye mada zinazofundishwa, Natarajia hivyo kutokana na umuhimu wake katika kuwasaidia viongozi hao, katika kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao, na hasa kuleta mabadiliko kwa kuhahakisha maendeleo yanapatikana.
Leo nitaangalia mada ya ukusanyaji wa taarifa / takwimu za awali Collection of Baseline data) kabla ya kuanza majukumu yao,hili nilishawahi kulijadili kwa ufupi mara kadhaa katika makala zangu, leo nitalijadili kwa upana kidogo kwa kuchambua sekta muhimu katika miradi ya kijamii ambayo ndio msingi wa mipango na bajeti katika halmashauri zetu,Nitajadili umuhimu wa takwimu hizi jinsi zinavyokwenda sambamba na mfumo wa kupanga mipango wa Fursa na Vikwazo ktk maendeleo (Opportunity and Objections to Development - O & OD planing methodology).
Makala iliyopita nilieleza jinsi diwani alivyo na sura sita katika utekelezaji wajibu na shughuli zake yaani, Diwani kama Mwezeshaji(Facilitator), Msimamizi na mtunga sheria ndogo (By laws), Msimamizi wa Ugawaji rasilimali, Diwani kama Kiongozi, Mwakilishi, Msimamizi wa Rasilimali za Umma . Leo Nitajadili ni kwa namna gani wajibu huo atautekeleza vema kwa kuhakikisha ana takwimu za awali za kata yake, pia kujua vyanzo vya mapato vya halmashauri, kwa kujua kila aina ya chanzo kina ingiza makusanyo ya shilingi ngapi? Na Kila Sekta ili pang wa shilingi ngapi kwenye kata yake na Halmashauri kwa ujumla.
Takwimu za awali ambazo ni muhimu diwani na hata wabunge kuzikusanya kwenye maeneo yao ni pamoja na;
1:SEKTA YA ELIMU
●Idadi ya watoto walioandikishwa katika shule za msingi
●Idadi ya shule za msingi na sekondari ktk kata
●Madarasa ya elimu ya awali
●Idadi ya watoto wanaoacha shule/Utoro (Pupils Absenteeism)
●Uhai wa kamati za shule kwa shule za msingi na bodi kwa sekondari
●Idadi ya wanafunzi kwa chumba cha darasa, yaani idadi pendekezwa ni 40:1
●Idadi ya mikondo
●Ubora na uwiano wa matundu ya vyoo (ratio pendekezwa ni kwa wavulana 1:25 na kwa Wasichana ni 1:20)
●Idadi ya vyumba vya madarasa na nyumba za waalimu
●Idadi ya madawati kwa kulinganisha na idadi ya wanafunzi (ratio pendekezwa ni 1:3)
●Umbali wa shule iliko ukilinganisha na makazi (hasa vijijini, na hata mjini mfano mtaa wa Kinyamwezi Kata ya Pugu manispaa ya Ilala)
●Idadi ya waalimu na madaraja yao (Ration pendekezwa ni 1:40)
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kuwa na takwimu za awali, ili iwe rahisi katika upangaji wa mipango inayohusu sekta ya elimu, ni rahisi kujua ukubwa wa tatizo (Magnitude of problem), Ni rahisi pia kupanga kiasi cha mafanikio tarajiwa baada ya mwaka au muda wako wa uongozi, ni rahisi pia kujua kata au jimbo lilikuwa wapi na sasa liko wapi.
Kumbuka kila item hapo juu itakupelekea kupata intervention ya kufanya.
2:SEKTA YA AFYA
Ni muhimu sana kujua takwimu zifuatazo zinazohusu upatikanaji wa huduma ya afya katika eneo lako kama diwani/Mbunge;
●Magonjwa makuu yanayosumbua/kusababisha vifo kwa wingi ktk eneo lako (Malaria, kuharisha nk)
●Magonjwa ya mlipuko mfano Kipindu pindu nk
●Magonjwa ya kuambukiza kama TB, Ukimwi nk (yako maeneo yameathiriwa sana na magonjwa ya kuambukiza na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya taifa)
●Idadi ya zahanati na vituo vya afya(both government and private owned health facilities) kumbuka manispaa huwa kuna maofisa wawili tofauti wanao shughulikia health facilities yupo anaeshughulikia za serikali na yupo afisa anaeshughulikia za binafsi.
●Idadi ya wauguzi na madaktari kwenye Zahanati na Kituo cha afya (Vya serikali), wahudumu wa afya ya uzazi.
●Idadi ya majengo na vyoo katika zahanati na vituo vya afya vya serikali)
●Usafi wa Mazingira katika makazi ya watu na maeneo ya sokoni.
3:MAJI SAFI NA SALAMA
●Vyanzo vya maji katika eneo lako (Mabwawa, visima vya asili, visima virefu vya pump za umeme au dizel, maji ya bomba kama dawasco, mito, maji ya mvua)
●Umbali kwenda kwenye vyanzo vya maji.
●Idadi ya kaya wanaopata maji ya dawasco majumbani
●Uhai wa kamati za maji
●Mahusiano ya kamati ya maji na WDC
●Uendeshaji na utunzaji wa miradi ya maji.
●Idadi ya kaya zinazopata maji safi na salama
4:HALI YA KIUCHUMI NA HUDUMA ZA UCHUMI
●Shughuli kuu za kiuchumi
●Taasisi zilizopo kwenye kata
●Barabara
●Vyanzo vya nishati
●Soko la bidhaa za mazao
●Eneo la Soko
●Huduma za Usafiri
5:SEKTA BINAFSI
●Karakana za ufundi/gereji
●Viwanda vidogo na vikubwa
●Hotel/Migahawa
●Vikundi vya uzalishaji mali
6:SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO
●Eneo linalofaa kwa kilimo na mifugo
●upatikanaji wa pembe jeo za kilimo na mifugo
●Idadi ya mifugo na wafugaji (kumbuka migogoro ya wakulima na wafugaji)
●Minada
●Majosho nk
Viongozi wetu wakikusanya taarifa hizo/Takwimu, zitasaidia kwenye upangaji wa mpango kwa kutumia O and OD, kwa kuangalia vipingamizi vya fursa ambavyo ni vikwazo, vitaondolewa kwa kuangalia vikwazo hivyo vinasababishwa na nini. Iwe ni ufisadi, fedha za mradi wa ujenzi wa Zahanati, madarasa nk ukijua nini kinasababisha kikwazo, basi kitakachofuata ni kuviondoa vikwazo kwa kupanga hatua za kuchukua.
Natarajia mafunzo haya yatajikita kwenye kuwajengea uwezo wa kutekeleza wajibu wao madiwani wetu katika sura 6 za diwani.
Tuwasiliane tena muda ujao