Mafunzo kwa njia ya vitendo..Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafunzo kwa njia ya vitendo..Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Easymutant, Aug 2, 2011.

 1. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Nimewaza sana na kufikiria sana na sipati majibu ya maana kabisa labda huku naweza kusaidiwa,
  lakini bado nina imani kabisa jibu langu nililopata ni sahihi kabisa Tanzania inaongozwa na Mwanafunzi ambaye yuko kwenye mafunzo kwa njia ya Vitendo, na wasimamizi wake sijajua wanamfuatilia vipi katika mafunzo yake ,mara nyingi sana wasimamizi hawa nawasikia tu kwenye vijiwe vya baa na sehemu tofauti tofauti kama kwenye dala dala wakimkashfu na kumtukana sana ..lakini sijawahi kusikia wasimamizi wa huyu mwanafunzi wakichukua hatua muhimu juu ya mwanafunzi wao...Mwanafunzi huyu ameshaharibu sana maabara na vitendea kazi alivyovikuta bila ya wasimamizi wake kufanya chochote, vichache tu vya muhimu ambavyo ameweza kuharibu ni Transfoma ya maabara ..mfumo wake ameuharibu kabisa kiasi kwamba umeme unawaka na kuzima bila taarifa na amewasababishia wasimamizi wake kukosa umeme na wanafunzi wenzake pia lakini bado tu hawamwambii kitu!

  Licha ya ukweli kuwa mwanafunzi huyu hakustahili hata kwa bahati mbaya kuwa katika mafunzo haya ya vitendo, na sijawahi kujua alipata vipi nafasi ya kuingia kwenye haya mafunzo (wasimamizi wake wanajua) kuna wanaopenda aendelee na mafunzo yake hadi amalize lakini pia wako wengi wasiopenda aendelee na mafunzo yake lakini wametulia tu utasikia wakilalama chini chini bila kuchukua hatua za vitendo,(rejea kelele za chura hazimnyimi Ngo'mbe kunywa maji)

  Mwanafunzi huyu licha ya jitihada za makusudi za kumfanya awe na japo na ka akili kidogo wasimamizi wake waliamua kumchanganya na vyuo vya nnje ili aweze angalau kuona cha kucopy lakini dah! amekuwa akiwaaibisha sana wasimamizi wake ..si utani huyu mwanafunzi ni wazimu sana inatakiwa uwe mwehu kuamini anachoropoka! wasimamizi wake walishabakishwa uchi mbele ya dunia nzima alipoulizwa kwa nini Chuo unachotoka ni Maskini walahi sikuamini eti HATA MIMI SIJUI...Juzi kati hapa alienda kumsabahi Mstaafu wa chuo hapo Bondeni jibu alilotoa ilikuwa bab kubwa...eti MIMI SITENGENEZI MVUA...huyu mwanafunzi si mchezo ni zaidi ya wazimu.. fundisha ujuavyo lakini ni SIFURI tena ile yenye masikio,

  Mwanafunzi huyu toka aanze mafunzo yake hapa chuoni ni dhahiri kwamba wanafunzi wenzake wanapata shida sana na ameshasababisha hasara nyingi sana kwa chuo hiki na wasimamizi wake wote, Cha ajabu bado wasimamizi hawa hawamchukulii hatua wamekaa kimyaa, Intake hii nayo ni hatari maana dah! wanafanyiwa kila aina ya ushenzi na mwanachuo huyu lakini walah wametulia! watalalamika mara moja tu kisha wanasahau ...mwanafunzi huyu huyu nasema ni hasara sana maana anasafiri sana ni TOURIST hatulii chuoni na kufanya anayotakiwa kuyafanya na wasimamizi wake mara nyingi hupewa majibu mepesi sana ...eti NISIPOSAFIRI wanachuo wenzangu watakufa njaa na msimamizi analizika na jibu hili..

  Mwanafunzi huyu ni mwoga sana katika kuchukua maamuzi na mwanachuo mwenzake alishamwambia kuwa huwezi kufanya maamuzi Magumu! ilibidi tu wasimamizi wengine wacheke tu maana huyu aliyemwambia ni mwoga wa kufanya maamuzi ni mwizi ile mbaya ..wanafunzi wenzake wanamjua anaiba hadi Pencil uzuri hachagui nani wa kumwibia anaibia hadi wasimamizi wake... wote hawa wako chuo kimoja na wasimamizi wao wanawapenda kweli yani...(ndo maana hawachukui action)

  Swali langu hapa ni kwa nini wasimamizi Hawachukui hatua juu ya wanachofanyiwa na wanachuo wa aina hii!????
  Angalizo: Unaweza kuendeleza tabia na mwonekano wa mwanachuo/wanachuo wa aina hii hapa!......
  Usisahau kulipa kodi ili TRA waendelee kukesha bar (Yes! sijawahi kujua kodi yangu inanisaidia nini na inafanya kazi gani)
   
 2. K

  Kiponya Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda Fasihi yako! Big Up Saaana!
   
Loading...