Mafundi Computer Naomba Tusaidiane Kuhusu hili

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,504
646
Nimepata msala kwa sababu ya kisimu kidogo tu cha vodafone na sasa nimekuwa kama mtu asiye na mikono.

Nimetumia computer tofauti tofauti kwa muda sasa, lakini sijawahi ku-short USB Ports kama ilivyonitokea juzi wakati najaribu kuflash kisimu cha vodafone ambacho kilikuwa kimeshaharibiwa kwenye sehemu ya kuchomeka USD cable.

Hivyo nikaamua kutumia ile shemu ya pinout au pin points, sasa kwa bahati mbaya PC yangu ikawa imepata short kwenye USB ports.

PC inafanya kazi vizuri tu isipokuwa haidetect chochote ninachokichomeka kwenye usb ports zote nne.

PC ninayotumia ni Dell Latitude D620.

Naomba msaada kwa yeyote aliyekwisha kupata msala wa hivyo na jinsi alivyoutatua.

Sent from my cupboard using mug.
 
Jaribu kuangalia kama kuna USB port ambayo kile ki plastic cha kati kimechomoka na nyaya zimegusana.

Mimi kuna Lenovo yangu moja ilinitokea hivyo, laptop ikawa haiwaki kabisa.

Nikachukua kitu chenye ncha kali nikatenganisha nyaya za USB zisigusane, zilikuwa kama zinatengeneza short circuit hivi.

Kama hicho ki plastic kipo vizuri na nyaya za USB port moja hazigusani, na USB ports zaidi ya moja zina matatizo, labda kuna kitu kingine kwa ndani kwenye USB hub ndiyo issue.

Ukiweza kuweka picha ya USB ports zilivyo sasa, itasaidia zaidi.
 
Jaribu kuangalia kama kuna USB port ambayo kile ki plastic cha kati kimechomoka na nyaya zimegusana.

Mimi kuna Lenovo yangu moja ilinitokea hivyo, laptop ikawa haiwaki kabisa...
Nashukuru mkuu, ngoja kesho nitaivalia njuga niisambaratishe yote nikague hivyo vitu ulivyoniambia.

Kisha baadaye nitaleta screenshot yake ili mui-analyze muone.

Wakati naisubiri kesho, kama kuna mwingine mwenye solution nyingine pia anakaribishwa ili kesho niziangukie zote kwa pamoja nikianza na hiyo ya Kiranga

Sent from my cupboard using mug
 
Hio d620 ina usb port 2 za kulia ambazo zinaweza kutoka maana ziko embedded kwenye motherboard. Sasa tafuta machine ingine d620 or d630 zinafanana hizo, toa hizo usb port weka huku ili ujue tatizo lina anzia wapi. Zikigoma tafuta mtaalamu ata loop njia huenda short imezikata electronics components zinazopeleka infor kwenye USB.
 
Mimi nahisi huenda niliua D+ na D- maana ukichomeka simu inachaji ila ni undetectable by pc.

Ngoja nifanyie kazi ushauri wenu wakuu tuone.

Sent from my cupboard using mug
 
Screenshots ni hizo wakuu pamoja na USB hub ambayo ni removable.
JPEG_20201214_092858_-1493201769.jpg
JPEG_20201214_092947_-1008269696.jpg
JPEG_20201214_093028_-2109335787.jpg

Sent from my cupboard using mug
 
Hiyo ic namba 2062 iliyo karibu na capacitor nayo naona ina mwonekano kama imebabuka na ina cracks kwa juu.

Iko karibu na inbuilt in usb ports.

Hivyo inabidi nayo nianze kuisaka.
JPEG_20201214_094034_-323822646.jpg

Sent from my cupboard using mug
 
Bwana Yesu Asifiwe Sana.

Nimefanikiwa kutatua tatizo baada kureplace ic mbili zenye namba 2062 ambazo nimezipata kwenye Dell moja hivi ka kizamani.

Kazi ya hizo ic ni BD2062FJ and BD2066FJ are dual channel high side switch ICs with an over- current protection for of. Universal Serial Bus (USB)

Hivyo basi Mungu awabariki sana wale wote mliotumia muda wenu kwa kunishauri na kunielekeza.

Da ishu solved;
Sasa hivi napambana kuirudishia bolt zake ili niendelee kula mzigo.

Kukutana na changamoto ni fursa, nimeepuka kununua PC mpya au motherboard nyingine, hapo nimejifunza kitu pia.

Safi sana mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom