Wakuu,mimi nimepona mafua kwa haraka sana kwa kufanya yafuatayo;
1. Menya kitunguu maji kisha chemsha kwa muda mpaka kilainike kiasi. Weka mchanganyiko huo kwenye kikombe cha chai na subiri upoe kisha kunywa kama chai ila usiweke sukari. Fanya hivyo angalau kutwa mara mbili.
2. Twanga tangawizi kiasi kisha chemsha,weka asali kidogo au sukari kisha kunywa kama chai kabla ya kulala na asubuhi. Tangawizi iwe kali kiasi cha kukufanya uweze kupiga chafya kidogo..sio kali saaana lakini.
3. Menya punje sita za kitunguu saum,katakata vipande vidogo vidogo kisha kama vidonge.
Ukifanya haya yote nakuhakikishia utaona tofauti kubwa sana siku yakwanza tu!
NOTE: Usitumie feni usiku wala AC..Epuka mazingira ya baridi baridi wakati wote,maranyingi uwezavyo.
Wapendwa msaada wa dawa nzuri na ya uhakika ya mafua.
Nimejaribu coldrill hayaponi.
Nimechemsha tangawizi,vitunguu saumu na limao lakini bado.
Uuuwiii nafwaa msaada plz.