Mafisadi wa ardhi wilaya ya Kinondoni

Mafisadi wa ardhi wilaya ya Kinondoni

anatory antony

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2014
Posts
324
Reaction score
254
Wana JF habari zenu,

Mnamo mwaka 2002 aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Yusufu Makamba alitangaza baada ya miezi sita kuwanyanganya ardhi wale waliokuwa wakimiliki mashambapori hayo kwenye kitongoji cha Kinondo Mashariki kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni iwapo hawatayaendeleza.

Baada ya muda uliotajwa kuisha Selikali ya kijiji cha mabwepande kupitia kamati yake ya mashamba pori walitekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa kwa kuwagawia wananchi waliokuwa wanahitaji ardhi.

Baada ya wananchi kugawiwa mashamba hayo waliyaendwleza kwa kufanya makazi yao ya kudumu.

Mwaka 2012 baada ya miaka kumi kupita tangu wananchi wagawiwe mashamba hayo, walijitokeza hao wanaojiita wenye mashambapori, walichoma nyumba za wananchi na baadhi yao waliuliwa na wengine kutiwa ulemavu wa kudumu.

Baada ya hapo wananchi walifungua kesi mahakama ya ardhi kanda ya Dar es Salaam, mahakama iliwaita Mara tatu wale wanaojiita wenye mashamba pori. Lakini Mara zote tatu hawakuitika wito wa mahakama.

Ndipo mahakama ilipotoa hukumu kwamba: Wananchi wasisumbuliwe tena na mtu yeyote, wana haki ya kujenga na kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Pili: mahakama ilitoa maelekezo kwamba wananchi wanaweza kuwafungulia hao wenye mashamba pori kesi ya madai.

Sasa jambo la kutia shaka ni kwamba mwezi wa sita mwaka huu 2017. Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Ally happy alitoa agizo kwamba ardhi ya Kinondo nayo ihakikiwe, na wale mashamba pori walioshindwa kesi mahakamani nao wahakikiwe.

Wananchi wanajiuliza swali, je Mkuu wa wilaya ya Kinondoni anatengua hukumu ya mahakama ya ardhi?

Ninakuomba Mh. Rais Magufuli pamoja na waziri wa ardhi Mh. Wiliam Lukuvi muingilie kati mgogoro huu wanaotaka kuingizwa wananchi wa kitongoji cha Kinondo mashariki.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda wachukue yale ya SUMAYE na viongoz wengne wa UKAWA
 
swala la ardhi limeshakua tatizo kuu hapa nchin, pamoja na serikali kua ndio wamiliki wa ardhi lakin walishashindwa kutatua migogoro ya ardhi. lakini hawa wenye ardhi kubwa ndio waasisi wa migogoro mingi.
 
Back
Top Bottom