Mafisadi kupata Uongozi ni dalili ya Udhaifu wa Sheria za Tanzania

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,851
Unapomuona Mtuhumiwa wa Escrow, EPA, Richmond/Dowans, Kiwira, Meli Chakavu, kuuza nyumba za serikali, Rada, Mabehewa fake, Kagoda, Meremeta n.k. anaendelea kupata dhamana ya Uongozi wa nchi bila kufikishwa katika vyombo vya Sheria, basi ujue upo Udhaifu kisheria wa hali ya juu sana.

Wahusika wa tuhuma hizi wanaeleweka na wamepewa dhamana ya uongozi wa nchi hii katika nyadhifa mbalimbali.

Ni Ushauri wangu tu kwamba, kama kweli tunataka kutumbua Majipu. Tutumbue mfumo wa Sheria za Tanzania kwa kuanza na Katiba Mpya, tena iwe ile ya wananchi a.k.a tuletewe ile ya Warioba.
 
Kama fisadi lowasa alivyokuwa anautaka urais kwa nguvu zote
Sheria ichukue mkondo wake. Kama ni mhusika afikishwe kwenye vyombo vya sheria na ahukumiwe kwa mfumo wa kisheria. Akiachwa basi ndio huo udhaifu wenyewe huo unaoongelewa.
 
Unapomuona Mtuhumiwa wa Escrow, EPA, Richmond/Dowans, Kiwira, Meli Chakavu, kuuza nyumba za serikali, Rada, Mabehewa fake, Kagoda, Meremeta n.k. anaendelea kupata dhamana ya Uongozi wa nchi bila kufikishwa katika vyombo vya Sheria, basi ujue upo Udhaifu kisheria wa hali ya juu sana.

Wahusika wa tuhuma hizi wanaeleweka na wamepewa dhamana ya uongozi wa nchi hii katika nyadhifa mbalimbali.

Ni Ushauri wangu tu kwamba, kama kweli tunataka kutumbua Majipu. Tutumbue mfumo wa Sheria za Tanzania kwa kuanza na Katiba Mpya, tena iwe ile ya wananchi a.k.a tuletewe ile ya Warioba.
Tatizo la nchi yetu siyo KATIBA peke yake ! Hata KATIBA iliyopo ikipata MTEKELEZAJI MWAMINIFU inafaa tu. Ktk nchi yetu kuna Vitu vingi sana vinafanywa kisiasa huku vikivunja sheria na KATIBA .
 
Tungekuwa na katiba nzuri marope angejiuzulu. Kwa katiba ya sasa anaonekana mjanja.
 
Back
Top Bottom