Mafao ya ustaafu kwa Wafanyabiashara

Mafao ya ustaafu kwa Wafanyabiashara

Gibiba

Senior Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
114
Reaction score
27
Hodii ndg zangu!

Kwa muda sasa nimekuwa natafakari juu ya hii mada lakini pia nilisubiria kama atatokea mbunge hata mmoja wa bunge letu tukufu angejaliwa kushukiwa na roho mtakatifu juu ya hili, lakini haijatokea.

Nimeamua kuwasilisha mwenyewe si kwa nia kukwamisha mapato ya nchi wala kuchochea kutoelewana kati ya serikali na wafanyabiashara hapana ni kwa nia njema kabisa ya kuijenga nchi yetu kasi, umoja na usawa kwa watanzania wote. Pia kutengeneza mazingira ya kunufaika kwa usawa kwa hawa wavuja jasho wote bila kujali makundi au aina ya kazi zao.

Si dhambi kwa mtu kuwa mfanyabiashara kama isivo dhambi kwa mtumishi na mfanyakazi.

Wafanyabiashara katika yetu wamekuwa wadau wakubwa na mstari wa mbele katika maendeleo ya kujenga nchi kwa vitendo. Si hilo tu, pia wanahusika moja kwa moja kwa kuhakikisha ufanisi wa maisha ya mtu mmoja mmoja kwa kila siku.Wanalipa kodi na tozo mbalimbali kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuendeleza Tanzania yetu sote.

Kodi hizi ndizo hujenga miundombinu ya barabara,elimu, afya, maji n.k. Lakini pia sehemu ya kodi hizi hulipa mishahara ya watumishi wetu wa kada mbalimbali ili kuhakukikisha maisha bora kwa watanzania wote.

Kama wanavyowekewa mafao ya ustaafu watumishi wa UMMA na SERIKALI, hivyo hivyo ningeshauri serikali kupitia Bunge letu tukufu, kuandaa na kupitisha sheria inayomwekea akiba mfanyabiashara anapokuwa kastaafu biashara aidha kwa kuamua mwenyewe, kufilisiwa, kufilisika au hata kupatwa majanga ya kuunguliwa moto n.k. Kwa kufanya hivi, serikali pia itakuwa;-

1: Imeweka usawa wa thamani ya hawa walipa kodi.

2: Mapato ya serikali kupiti kodi yataongezeka, wafanyabiasha watalipa kodi kwa halali na hiari kwa kutambua umuhimu wa kujiwekezea kwa baadaye.

3: Kama sii kuisha, wakwepa kodi watapungua kwa kiasi kikubwa.

4: Itatoa urahisi wa makadirio ya kodi kwa TRA kuliko sasa ambapo naamini wafanyabiashara wengi huficha thamani ya miradi halisi wanayomiliki kwa kuhofu kulipa viwango vikubwa.

4: Sekta ya viwanda itajichochea yenyewe.

5: Kilimo na ufugaji vitakuwa vyenye tija zaidi kuliko sasa. Watu watalima na kufuga kitaalamu na ubunifu zaidi.

Kwa kufanikiwa haya, naamni ongezeko la makusanyo ya kodi ya serikali yatapanda kwa kiasi kikubwa sana bila kutumia nguvu wala gharama yoyote.

Ni mtazamo wangu tu,wenye nia njema kabisa ya kuunga juhudi za maendeleo ya nchi yetu sote.

"TANZANIA ITAJENGWA NASI SOTE" Anza leo

Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo zuri na nashauri lifanyiwe kazi na bunge letu.

But....

Kuwe na kipengele cha kukubali au kutokubali kuongezewa tozo ya kodi (kipengele muhimu sana)



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom