Mafao ya Kupoteza Ajira

Mafao ya Kupoteza Ajira

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
10,700
Reaction score
14,766
Hii ndio ile inaitwa thubutu kulima utalima kwa kuteseka harafu bei unakuja kupangiwa na madalali wa mjini...tumewakosea nini hawa viongozi wetu, kosa letu sisi kweli ni huu utanzania au kuna jingine...?

Mafao ya kupoteza ajira hutolewa kwa mwanachama wa NSSF aliyepoteza ajira kwa kuachishwa kazi au ajira yake imefika ukomo kwa sababu yoyote ile isipokuwa kwa kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe (Resignation).
Mafao ya kupoteza ajira hutolewa kwa mwanachama aliyetimiza vigezo vifuatavyo;
  • Mwanachama awe amechangia kwenye Mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na nane (18)
  • Awe mwanachama wa NSSF aliye poteza ajira kwa kuachishwa kazi au ajira imefikia kikomo kwa sababu yoyote ile isipokuwa kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe (Resignation)
  • Awe ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Asiwe na sifa ya kulipwa mafao ya muda mrefu ambayo ni Pensheni ya uzee, ulemavu au urithi/wategemezi
  • Ithibitishwe kuwa mwanachama hayupo kwenye ajira yoyote
  • Awe na umri chini ya miaka 55.
Mafao yanayotolewa kwenye fao la kupoteza ajira
  • Mwanachama atalipwa asilimia 33.3 ya mshahara wake aliokuwa anapata wakati akiondoka kwenye ajira. Malipo hayo yatalipwa kwa kila mwezi mfululizo kwa kipindi kisichozidi miezi sita ndani ya mwaka mmoja. Malipo ya kila mwezi yatakoma iwapo mwanachama atapata ajira
  • Mwanachama ambaye atakuwa hajatimiza michango ya miezi 18 atalipwa mkupuo wa asilimia hamsini (50%) ya jumla ya michango yake.
Ukomo wa Mafao ya Kupoteza Ajira
Iwapo mwanachama ataendelea kukosa ajira baada ya kuisha kwa kipindi cha miezi 18, anaweza kuwasilisha maombi kwa Mkurugenzi Mkuu ili baki ya michango yake ihamishiwe kwenye mpango wa uchangiaji wa hiari atakaouchagua mwenyewe ili aendelee kuchangia kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mpango husika.

4.0 Tahadhari
Ni kosa la jinai chini ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018, kwa mtu yeyote kwa makusudi kutoa taarifa za uongo/ zisizo sahihi kwa lengo la kujipatia mafao yeye mwenyewe au mtu mwengine.
 
Mkuu vip ulifanikiwa kulipwa??
Atusaidie tufahamu maana Mimi mwenyewe nimeandika barua ya kuhamisha michango yangu kwenda kwenye mfumo wa uchangiaji wa hiari. Je nitafahamu vipi kuwa michango yangu imeshahamishwa maana ni mwezi Sasa sijapigiwa simu yeyote na PSSSF
 
Uliandika barua mkoa gani mkuu? Mimi mwezi wa tatu niliandika barua ya kuomba kuhamisha malipo kwenda kweny uchangiaji wa Hiari haikupita week 2 nikapigiwa simu na kutumiwa sms nikajaze fomu za withdrawal benefits supplementary.
Fomu nilijaza tarehe 22 mwezi wa 3 ila Juzi nimepokea muamala kwahiyo ndani ya miezi miwili jamaa wanaeza maliza kama documents zako zimenyooka.
 
Mkoa wa Geita mkuu!
Niliandika barua toka tarehe 8/04/2025 lakini sijapata notification yoyote hadi muda huu
 
Uliandika barua mkoa gani mkuu? Mimi mwezi wa tatu niliandika barua ya kuomba kuhamisha malipo kwenda kweny uchangiaji wa Hiari haikupita week 2 nikapigiwa simu na kutumiwa sms nikajaze fomu za withdrawal benefits supplementary.
Fomu nilijaza tarehe 22 mwezi wa 3 ila Juzi nimepokea muamala kwahiyo ndani ya miezi miwili jamaa wanaeza maliza kama documents zako zimenyooka.
Mimi nilijaza Toka mwezi wa 5kimya!
 
Vip mkuu
Hizo document ulizojaza kuna sehemu ya mwajiri tena kuthibitisha? Naomba msaada mkuu
 
Back
Top Bottom