Jayspeed
Senior Member
- Feb 23, 2014
- 156
- 169
Napoandika haya sio kuwa najua sana ila kias nachojua nashirikisha wanajamii wenzangu.. Nlipokosea tukosoane tufundishane ili kuongeza uelewa kwa wengine...
.
Mafanikio ni kama chakula ukipendacho, na wabaya wako ni kama chachu".
Hakuna binadamu ambae amefanikiwa kirahisi yaani moja kwa moja bila kukutana na changamoto za walio mzunguka, na changamoto hukuacha wewe ufanye maamuzi aidha ya kuzikabili au kuzikimbia na unapozikimbia inaonyesha umekata tamaa na wabaya wako hufurahi.. Tambua:
1: Katika maisha yako tambua kuna watu watakua na wewe bega kwa bega kila nyakati zako zote za maisha, hawa hukujali kwa kila nanma sio kipindi cha tabu wala cha mavuno sio kipindi cha kupanda wala kushuka hawa wapo na wewe kila siku na kila nyakati. (Wakumbatie vizuri)....
. 2: Kuna watu ambao watakuwa na wewe wakati wa mafanikio tu ili waweze kupata starehe, hawa hukuacha upambane na changamoto zako mwenyewe kisha ukimaliza waje wale matunda.(ishi nao kwa akili)...
.
. 3: Kuna watu ambao watakuchukia mwanzo hadi mwisho bila kujali mazuri mangapi umefanya na unaendelea kufanya (wachukulie ndio chachu ya mafanikio yako).. watu hawa hawapendi kuona umefika sehemu fulani au umefanya mambo makubwa hata kama ni mazuri kiasi gani sababu wanapenda kuona upo chini yao kabisa, watu hawa ishi nao sababu wanakupa nguvu ya kutafuta kila siku bila kichoka Usiwachukie sababu hawa ni moja ya watu ambao wapo kwenye maisha yako kama kukufunza mbinu mpya za maisha na kukuonyesha ni wapi uongeze juhudi.....
"Behind every successful person lies a pack of Haters!" Aliwahi kusema mwandishi na mjasiriamali mmoja Gloria Tesch Hivyo tambua mafanikio yako yanajengwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo wanaokuchukia..
Mungu akubariki.