Vyama vya siasa nchini Tanzania tangu vianze vimeleta demokrasia hasa ktk uhuru wa kutoa mawazo, raia kujua haki zao nk lakini lengo kubwa nafikiri ilikuwa pamoja na hayo kumletea mawananchi maisha bora jambo ambalo halijafanyika ipasavyo na ili unuse harufu ya maisha bora ni lazima uwe member wa chama fulani, kinyume na hapo utapata kwa taabu harufu hiyo imefika wakati tuwe na katiba inayobana kiongozi kuleta mabadiliko ktk maisha ya mtanzania kama kweli tunajenga nyumba moja basi tuwe na serikali ya mseto kwa vyama vyote kupewa nafasi ktk uundaji wa serikali baada ya chama fulani kushinda na hii iwekwe ndani ya KATIBA mpya.