Mafanikio ni uamuzi

Apr 18, 2017
22
8
“Katika mafanikio ni ngumu sana kumzuia mtu anaejua wapi anakwenda na nini anakitafuta kwenye maisha yake ”


Na Humphrey Gasper,

Katika maisha watu wengi wanapenda kufanikiwa na sio kutafuta mafanikio, ilihali kufanikiwa na kutafuta mafanikio ni vitu viwili visivyolandana.


mafanikio ni uamuzi ni nini haswa..?

Kufanikiwa na kufeli ni maamuzi ya mtu mwenyewe,kufanikiwa kuna nguzo kuu tatu muhimu

malengo

mwelekeo

kujituma,

mtu mwelekeo sahihi wa nini haswa anakitaka katika maisha yake, wapi haswa anatamani kuwa au kwenda katika maisha yake na kujituma katika kazi zake au masomo huyo ana nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa katika maisha kwa kuwa anayatafuta mafanikio hii ni sababu nimeanza kwa kusema mafanikio ni uamuzi.


Mtu anaejua wapi anakwenda na nini anakitafuta kwenye maisha yake ni ngumu sana kumzuia katika mafaniko,

maisha ni kama kitabu,kuna kurasa zingine ni za furaha,huzuni na za kusisimua pia, usipofungua kurasa inayokuja huwezi kufahamu kilichoandikwa humo.


NGUVU ZETU PEKEE HAZITOSHI.

Katika kuyatafuta mafanikio kuna vikwazo vingi, kuna kukata tamaa lakini kuna nguzo muhimu sana katika yote ambayo ni imani kwa Mwenyezi Mungu, nukuu

"kama Mungu yupo upande wetu ni nani wa kutuzuia ” -warumi 8:31

yatupasa tutambue fika kwamba Baraka na neema zinatoka kwake aliyetuumba hivyo basi imani ni ya msingi katika kuyatafuta mafanikio.


nafasi itakayo kuwezesha kufanikiwa ni ile unayoogopa kuitumia, wakati ni sasa unasubiri nini,,? unachelewa!


“usitegemee sana kuaminiwa na watu wengine kabla haujajiamini mwenyewe ”amini katika uwezo wako utafanikiwa.


MAFANIKIO NI UAMUZI.



for more of this you can

follow us on

instagram: @kingkid8

Twitter: @officialhumph

Whatsapp: 0763034980
 
Back
Top Bottom