Maendeleo ya Tanzania na siasa zake

NKWENYE

Member
Feb 19, 2017
57
183
Ndugu wanabodi kabla sijaingia kwenye lengo lenyewe naomba ninukuu kauli ya mwanasayansi mmoja(sitamtaja maana namwamini kwa nafasi yangu). Aliyasema haya "SIYO KWAMBA WAZUNGU WANA AKILI SANA KULIKO WAAFRIKA, HAPANA, ILA WAZUNGU HUMSAIDIA MJINGA KUJINASUA KUTOKA KWENYE UJINGA ALIONAO MPAKA KUWA MWEREVU WAKATI AFRIKA WAEREVU WOTE HULAZIMISHWA KUWA WAJINGA"

Baada ya nukuu hiyo niingie kwenye mjadala wangu..
Ni takribani miaka miwili sasa toka serikali hii tukufu ishike madaraka. Lakini mpaka leo nchi hii imekosa LESSON PLAN.
haijui ifanye nini, wakati gani, na kwa muda upi... Kwa mfano. Tupitie wizara chache muhimu.

NISHATI NA MADINI.
Hii wizara mpaka leo umeme siyo wa uhakika, bei ya umeme tulitarajia ishuke zaidi ya hapa kutokana na ugunduzi mkubwa wa gesi nchini lakini hakuna

ELIMU.
Huku ndo ziro kabisa, mikopo ya wanafunzi hakuna, watoto mpaka leo wanakaa chini, walimu wa sayansi hakuna, mishahara kwa walimu hovyo, miundombinu yote sifuri,miongozo ya hovyo kila siku.

VIWANDA
Mwijage sijui yuko wapi siku hizi.. Hadi viwanda vinaandika nembo ya Kenya waziri yupo tu. Kwa ujumla huku kwenye kaulimbiu ya serikali yetu ya SERIKALI YA VIWANDA ndo kulipaswa kuwekewa mkazo lkn cha ajabu tuna kiwanda cha kusaga mapera cha bakhresa..

MALIASILI
Huku watalii ndo hatuwaoni kabisa kama zamani.. FARU JESCA sijui kaishia wapi..

AJIRA
Vijana wanaambiwa wajiajiri tena kwa mbwembwe.. Ajira zimesitishwa, walioajiriwa matumaini yamepotea. Hovyo

SHERIA NA KATIBA
Hahahahaha.. Hapa naomba mchangie maana ndo kwenye uchochezi... Huku ndo kumekanyagwa kuliko sehemu yeyote ile..

Kwa uchache tu, lazima akina LIZABONI tukubaliane kuwa nchi yetu kwa sasa haina mwelekeo. Nchi nzima imehamia kwenye kupambana na watu WEMA wanaoikosoa serikali.. Watu wanaoikumbusha serikali mambo ya msingi... Mkiambiwa nchi ina njaa mnawakamata wanaosema wakati ni kweli njaa ipo.. (ref:mbunge wa shinyanga mjini), mkiambiwa hamna uwezo na mikakati imara ya kupambana na madawa ya kulevya mnasema wanaosema hivo wanayauza!! Mkiambiwa vijana hawana ajira mnawaambia wakajiajiri wakati mnaosema hivyo mmeajiriwa! Kila mnachoambiwa kwenu ni dhambi..

Mwisho : Watanzania tunaomba akina LIZABONI mtupe vipaumbele vya serikali For the few two years remaining! Na mtuambie mnatekelezaje.. Achaneni na akina LEMA, mnawapa kura nyingi mno chaguzi zijazo kwa kuwaweka korokoroni kila siku..

Madawa ya kulevya mmeshafeli tayari, uhakiki umewashinda maana huwezi hakiki vyeti ambavyo viko kwenye mfumo wa kikompyuta kwa mwaka mzima.. Mnajificha kwenye karanga...
Asante

NKWENYE. (Mtu wa kawaida kabisa).
 
mkuu kwani nini maana ya "acha waisome namba eee..?"
binafsi sidhani kama wazungu wanatubagua kwa rangi yetu tu!,naona jambo hili linachagizwa na tabia zetu ubinafsi,kutojali,ujingan.k...

wasomi tunaowategemea ndio wakandamizaji walio tuelemea nini maana ya usomi wao..?
uongozi si jambo lakukurupuka linahitaji mtu mfikiriaji mwenye majibu sahihi yaliyoambatana na vitendo,mzalendo,mwaminifu,muelewa n.k

katiba ni maneno tu yanaweza yasifuatwe na katiba bila uzalendo ni sawa na kumwagia maiti maji et iamke!!
tunahitaji kuwa na chombo imara cha nchi kitakachosimamia mambo yaende ktk mstari ila hili linahitajika liundwe na watu waaminifu na wazalendo lkn wapi tawapata..? wachache wanajali wengi wanataka mali.
kunahaja ya kusambaratisha na kuunda upya
 
Back
Top Bottom