Maendeleo ya Michezo Tanzania

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Hivi karibuni Rais SSH alipokea kombe la mpira la dunia, swali la kujiuliza je, kuna mazingira wezeshi ya kukuza na kuendeleza vipaji nchini?

Kila kona ya nchi, mijini hadi vijijini, wananchi hukusanyika palipo na TV kuangalia mashindano mbali ya michezo ndani na nje ya nchi. Huu ni uthibitisho kuwa michezo ni moja ya starehe kuu ya watu. Ili basi, kuweza kupata wachezaji wazuri wa kuliletea Taifa heshima katika michezo, yafuatayo yawezekana kufanyika:

1) Wizara husika, hasa ya Ardhi, ihakikishe kila shule inatengewa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya michezo.

2) Ujenzi wa viwanja vya michezo kila shule na vyuo nchini ili kuibua na kukuza vipaji. Hili linawezekana ikiwa kila Hamashauri itatenga angalau silimia 2 ya mapato yake kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya michezo.

3) Wizara husika ziandae mitala ya masomo ya michezo na walimu/wakufunzi.

4) Kuhamasishwe ujenzi wa viwanda vya vifaa vya michezo.
 
Back
Top Bottom