Roger Sterling
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 13,012
- 23,625
Katika hotuba yake ya jumatatu, Rais Magufuli alitoa rai(?) kuwa watanzania tuache 'udaku' na 'viposti posti', na badala yake tujikite katika kujadili habari zitakazoleta maendeleo katika nchi. Rai hiyo ilikuja baada ya karibu pande zote za nchi kujikita katika kujadili vitendo vilivyofanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, bwana Paul Makonda katika jengo la Clouds Media.
Hata leo katika mijadala mbalimbali kuhusu yaliyotokea, watetezi wa Magufuli na Makonda wanasisitiza tuyaache ya Makonda na kujadili maendeleo. Sasa kwa niliye slow kidogo katika kuelewa mambo, naomba kueleweshwa zaidi kuhusu hayo maendeleo.
Je?
Kujadili na kuhoji kuhusu matumizi ya rasilimali na kodi za watanzania katika mambo binafsi ya viongozi wa umma si maendeleo?
Kujadili na kuhoji uhuru na usalama wa vyombo vyetu vya habari si maendeleo?
Kuhoji na ketetea usalama wa wananchi kwa ujumla siyo habari za maendeleo?
Kuhoji usawa na haki kwa watanzania wote bila kujali imani, hadhi, kabila, nafasi, n.k, hayo si maendeleo?
Kujadili na kuhoji maadili na utashi wa viongozi wa umma si maendeleo?
Ni maendeleo gani tunayoshauriwa/amriwa kujadili, ambayo tunaweza fumbia macho usalama wetu kuwa mashakani, ukosefu wa haki na usawa, ukosefu wa uhuru kwa vyombo vya habari, kauli za kejeli na kukatishana tamaa, n.k.??