Maendeleo na figisu za Serikali

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,554
Reaction score
4,171
Ni muda mrefu tangu kupita kwa umeme kjijini kwetu(nilipo kwa sasa)bwana mmoja akatoa ufadhili wa Transfoma na nguzo. Alichoahidiwa angefungiwa tangu June. Akatoa kipaumbele kwamba waunganishe kwanza zahanati ni ya Serikali pamoja na shule halafu nyumbani kwake. Hizi zote ni gharma zake wala hakuomba Rea.Na hii transfoma ipo alikuwa anaitumia kwenye plant take.

Mafundi wakaja kupima na ikawa ni kuambiwa kesho...kesho, Miez 2 ikaisha. August akaja mbunge Bukwimba akapita vijiji vyote akasema ameingiza vijiji hivi kwenye mpqngo wa REA hivyo tutulie. Alikuja na jamaa akasema yeye ni fundi toka TANESCO na mwezi ujao mambo yatapendeza.Walikuwa faya hata maswali hawataki.

Leo Novemba hatuoni hata dalili ya umeme.

Serikali haitaki kuonekana imeshindwa kuhudumia wananchi.Akitokea mfadhil mpeni nafasi .Tunaona Sheria zinavyowekwa sawa ili kuwanyonga wanaouza maji Dar.

Wauza Simu, redio, TV, madishi na mafundi wake rungu laja
 
Msilaumu kila jambo Kuna swala la logistic, REA wana mpango kazi, pia huo msaada huenda ukawa faida ya mzabuni kwani bajeti yake ipo tayari
 
Msilaumu kila jambo Kuna swala la logistic, REA wana mpango kazi, pia huo msaada huenda ukawa faida ya mzabuni kwani bajeti yake ipo tayari
Kwann gharama yake hiyo isiingie kwenye maendeleo ya kijj? Huyu aka fungiwa kwa gharama zake....au gharama itkayotumika ipunguze ile 27000 ya kuunganishia.
Mkuu hii ni figisu
 
Nani wa kusimamia transaction hiyo!? Una hakika ubora transfoma husika!? Vipo vingi vya kusaidia madarasa,zahanati nk ngazi ya vijiji.
 
Nani wa kusimamia transaction hiyo!? Una hakika ubora transfoma husika!? Vipo vingi vya kusaidia madarasa,zahanati nk ngazi ya vijiji.
Aliinunua kwa matumizi ya plant yake (pa kuchenjulia dhahabu)ni 10kvw
Bado inafanya kazi. Aliamua kufunga ile plant.
Na mafundi walishapima wakaridhia wakaambiwa kufuata kibali wilayani....mkoani....office ya ccm mkoa...
.ilikuwa balaa..

Shuleni amefadhili kufyatua tofali 6000 Na kujenga darasa 2 hadi kumaliza. Hii ni kwa shule 2 pamoja Na samani za sh 960,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…