Maendeleo katika mizania Tanzania

Doncho kun

Member
Jan 11, 2019
11
10
Maendeleo, Maendeleo!
Kumekuwa na maoni mengi juu ya "maendeleo" bila kutajwa hasa ni wap au nini kinazunguzwa, pia wengine wakizungumzia maendeleo kwa upande mmoja tu unaoweza kuonekana dhahiri kw macho kama kujengwa kwa barabara mijini na vijijini, kujenga hospitali na vituo vya afya, kujenga madaraja, madawati mashuleni, kununua ndege n.k. Ni kawaida binadamu tukawa tunapenda kusikia tunachokipenda tu kila wakati na ni wachache wenye moyo wa kuvumilia wasichokipenda kupata kusikika. Ndioo, tumeshuhudia maendeleo ya watu yakiwa hayatiliwi maanani, thamani ya utu ipo chini sana nadhani kwa nchi nyingi kuwa na utawala wa sheria, haki za binadamu (uhuru wa maoni, haki za faragha ,imani n.k), mfumo mzuri wa elimu, uswa ktk ajira, haki za kisiasa n.k, hivi vyote watu hawavioni kama ni maendeleo badala yake wapo wanaotamani hivi vyote wananchi wasivipate ila tu barabara zijengwe, madawati, madaraja n.k. Kwa mfano kwenye vikao vya bunge hivi karibuni nimemsikia Mbunge Mh. Joseph Kasheku (Msukuma) akilalamika kuna shule jimboni kwake ina wanafunzi elfu tatu na mia tano (3,500) huku pakiwepo tu walimu tisa (9) halafu bado kuna watu wachache wanaosema elimu bure na kuleta madawati shule ni maendeleo kamilifu na yanaimbwa kwa nguvu nyingi huku tukishindwa kuboresha miundombinu ya kuchagiza maendeleo ya watu.

Nikirudi upande wa wanaoongozwa, ni kawaida yetu kuitaka serikali kuleta maendeleo (ktk nyanja zote) bila kutathimini wajibu wetu kwa serikali kwa kulipa kodi,ada na tozo mbalimbali zilizopo kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea tukitaka maendeleo hatuna budi kutekeleza wajibu wetu. Ni kweli kabisa kumekuw na utitiri wa kodi, ada na tozo kitu ambacho kinapelekea ukwepaji. POINT: point yangu ni kwamba huu ni wakati Wananchi tuanze kupigania maendeleo ya watu ili tuweze kutekeleza wajibu wetu kwa taifa ikiwemo kulipa kodi n.k. lazima tupate mitaala mizuri ya elimu ili tuzalishe watu wenye ubora kw mazingira ya Tz, mashuleni pawepo na walimu wa kutosha na walio na ubora, tuwe na vyombo huru vya kutenda haki kwa usawa bila kujali hadhi na tuwe na katiba madhubuti ya kusimamia na kuthibiti nchi
 
Back
Top Bottom