MKAKATI WA KULETA MAENDELEO KATIKA JAMII
Maendeleo ni nini?
Maendeleo ni hali au mchakato wa kukua/kuboreka kwa jambo Fulani. Hii inaweza kukua/kuboreka kwa Elimu, Mazingira, Afya, Uchumi, Uslama, Miundombinu na mengineyo.
Chachu ya maendeleo
Chachu ya maendeleo inaanzia kwenye nafsi ya mtu mmoja mmoja kwa kukerwa na au kutoridhishwa na jambo fulani na kuamua kwa dhati ya moyo wake kulitafutia ufumbuzi. Hakika nafsi hii moja kwa kuungana na nafsi nyingine zenye mueleko unaofanana (kukereka na kutoridhika na jambo kama hilo au jingine) imani yangu ni kuwa maendeleo yanapatikana.
Nani analeta maendeleo?
Kwa imani iliyojengeka kwa wananchi kwa muda mrefu ni kuwa maendeleo yanaletwa na Wanasiasa/Serikali kama vile Diwani, Mbunge, Waziri, Serikali ya mtaa au serikali kuu. Kwa kiasi fulani imani hii ni sahihi, lakini je kama hakuna nia na muungano kutoka kwa wananchi wenye kukereka na kutoridhika kwa jambo fulani kwa uwazi maendeleo yanakujaje? Usahaulifu, Dharau na Ubinafsi ni hulka ya binadamu na ni kikwazo cha maendeleo, inahitaji umoja wetu wananchi kuikumbusha na kuielekeza serikali na pia kukumbushana na kuelekezana sisi wenyewe wananchi kuhusu kero zetu zinazotukabili.
Kwa mfano; Mtu mwenye fedha anaamua kumpeleka mwanae shule ya mbali na kulipa pesa nyingi ilhali jirani kuna shule ili kutafuta elimu bora. Kwa umoja wetu wananchi tunaweza kuwekeza na kuboresha shule zetu kwa kushirikiana na serikali. Hailazimishwi kumsomesha mtoto popote mtu atakapo, lakini kwa nguvu ya wananchi tunaweza kuboresha maisha ya walimu, kuboresha mazingira ya kusomea, kuboresha maktaba na maabara za shule ikiwa tutaamua na kuungana.
Je vipi kuhusu ulinzi na usalama wa raia na mali zake? Wananchi tunafanya nini kuhakikisha hali hii inaboreka? Tuna ukaribu kiasi gani na maafisa wa ulinzi na usalama na raia? Uhusiano ulio mwema katika ya maafisa hawa tumewaachia wahalifu na sababu hiyo wahalifu wanfaidika na mhusiano hayo na kuwa kilio kwa raia wema. Hatuwezi kubadilisha mahusiano hayo yakawa kati ya maafisa hao na raia wema badala ya wahalifu? Ni wangapi miongoni mwa wananchi wanamfahamu hata kwa sura angalau afisa mmoja wa ulinzi na usalama wa raia katika katika kata au mtaa wake?
Nini cha kufanya?
Kuunganisha nguvu zetu wananchi kuanzia ngazi ya mtaa na kuendelea kwa kufanya yafuatayo;
1. kuikumbusha serikali na wadau wengine kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa pamoja na sio kuishia kulalamika kila mmoja kivyake au kwenye mabaraza ya soga kama vijiweni, kwenye mabaa na kwenye mitandao ya kijamii bila kufikisha mahala husika.
2. Kuongea na wahusika kama vile walimu na wanafunzi katika suala la elimu, maafisa usalama wa raia na mali zake katika suala la ulinzi na usalama, mabibi na mabwana afya katika suala la mazingira na afya na kila anaehusika katika jambo lenye manufaa kwa jamii kuhusiana na changamoto zinazowakabili na nini kifanyike kuzikabili changamoto hizo.
Maoni yangu
Tuanzishe utaratibu wa kukutana na kuzungumzia kero mbalimbali zinazotukabili na namna bora ya kuzitatu. Ni kwa umoja wet utu bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa na kidini ndio tunaweza kujikwamua katika kero hizo.

KWA PAMOJA TUNAWEZA.