Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Wakati hali ya ukame ikiwa imeitesa sana sehemu kubwa ya Somalia, miaka zaidi ya ishirini iliyopita, taasisi ya umoja wa mataifa kuhusiana na chakula, ilipeleka helikopta zilizokuwa zikidondosha mifuko ya mahindi na chakula kingine. Watu waliigombea sana mifuko ile ili kuweza kuitibu njaa ya muda mrefu. Wageni waliopeleka chakula katika eneo lile wakalazimika kuwepo kwa muda mrefu ili kutoa msaada kwa zile kaya ambazo zimedhoofika kwa njaa. Kilichowashangaza wageni wale ni kuwa baada ya watu kuanza kupata nguvu, wakarudia tena kwenye siasa zao za chuki na uhasama wa kikabila na kikanda. Lakini wakati njaa imetawala wote walikuwa tayari kutazama juu ili wajiweke tayari kupokea chakula kilichokuwa kikidondoshwa kutoka kwenye helikopta.
Maisha ya binadamu huwa na mahitaji mengi, na yanafanana haswa kwa nchi kama Tanzania. Shida za maji zilizo katika sehemu kame kama vile katikati ya nchi, hazipo katika eno hilo tu. Shida za umeme, shida za barabara mbovu, zipo nchi nzima. Maendeleo ya kweli hayaendani na siasa za uhasama za vyama vya siasa. Hospitali zikiwa bora, watakaotibiwa ni wana CHADEMA, CUF na CCM. Elimu ikiwa bora watakaoleta maendeleo ya kisayansi ni watoto wa wafuasi wa vyama hivyo.
Maendeleo ya kweli hayana chama, shida za kimaisha hazibagui chama, zipo kila kona ya Tanzania. Hulka za kutazamana kivyama, kubaguana, kutesana, kutaka kuwekeana sumu kwenye soda ua maji, ni vitu ambavyo tunaweza kuvifanya kwa sababu tu ya kutouelewa ukweli kwamba ustawi wa jamii yenye amani, ni kitu chenye thamani kuliko kujitambulisha kwetu kwa kutumia itikadi. Tena kwa bahati mbaya itikadi hizo tumeziiga kutoka kwa wazungu, hatuzifahamu kwa undani. Bado sisi ni wanafunzi wa somo linaloitwa siasa lakini tayari tumeshautanguliza uhasama kiasi cha kusahau kuwa maendeleo ya kweli huwa hayana chama, wala hayambagui mtu kwa sababu ya imani yake katika itikadi fulani.