Maelezo ya wenye nyota ya Simba

Maelezo ya wenye nyota ya Simba

kichakaa man

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
5,497
Reaction score
5,186
MAELEZO YA NYOTA YA SIMBA LEO

Hii ni nyota ya Tano katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Julai na 22 Agosti au wenye majina yalio anza na herufi E na Q.

waliozaliwa kati ya Tarehe 21 July na 20 August Asili yao ni Moto. . Sayari yao ni Sun (Jua). Siku yake nzuri ya bahati ni siku ya Jumapili, Namba ya bahati ni 1 na 4 .Malaika wake anaitwa Michael au Raukayaeel na Jini anayetawala Jumapili anaitwa,

Abdulahi Saeed al Madhhab au Och Herufi ya Jumapili ni F

Rangi zao ni rangi ya Dhahabu (Gold), Nyekundu (Red) na rangi ya Machungwa (Orange) Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri kama Dhahabu na Njano nzito au iliyoiva.

Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Nyeusi, Bluu iliyoiva (Indigo) na Bluu ya Samawi (Ultramarine).
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni, Njano (Yellow) na Njano-Machungwa.

Kito (Jiwe) ni Amber, Chrysolite, Yellow Diamond, Petrified Wood Garnet, Diamond, Jasper, Quartz na Onyx.

Madini yao ni Gold (Dhahabu). Manukato yao ni Maski (Musk) na Uvumba.

MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya Nyota hii ni Uimara na Kutokubadilika.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni Unyenyekevu.

Maadili yao ni Uwezo wa Uongozi, Kujiamini, Ukarimu, Ubunifu na Kupenda raha.

Matakwa yao ni Starehe, Haja ya Kung’ara mbele za watu na Kujikweza.

Tabia za kujiepusha nazo ni Kujisifu, Kiburi na Kuamrisha.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Mshale.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Nge na Ndoo.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Nge.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mashuke.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mshale.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ndoo.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mshale.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Punda na Kaa.

KIPAJI CHA SIMBA:
Simba wana kipaji cha ufunuo wa kiungu , wana uwezo wa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwaletea fedha pamoja na kwamba hazikai.Wanauwezo vilevile wa kuponya kwa kutumia mikono yao kuponya watu na wanakipaji cha asili cha uongozi. (inspired):

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Simba ni watu wanaopenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Wanapenda kutumia na wanataka waonekane kwamba wana hali nzuri, wanapenda sana kuheshimiwa.
Jambo kubwa walilonalo ni uwezo wa kuvumbua mambo ambayo watu wengine hawajui.

Ni watu wakarimu lakini wajeuri na wanapenda sana kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.Tabia yao ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanaowapenda.
Furaha haina mpaka katika mapenzi ya Simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu. Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza.

Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika inakua vigumu sana kuyatengeneza.

Tatizo lao kubwa ni kujisahau Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.

KAZI NA BIASHARA ZA SIMBA:
Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi zifuatazo; kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.Wanatakiwa wafanye kazi za usonara au kazi za kuuza au kutengeneza mavazi ya mitindo.Vilevile wanatakiwa wafanye kazi za uigizaji au uendeshaji sinema au kazi zozote zinazohusika na masuala ya vijana.Kazi yao nyingine ni ya ualimu katika taasisi, shule au vyuo vya ualimu.

MAVAZI NA MITINDO:
Simba mitindo yao iwe ya kifalme, Kitajiri na inayoashiria nguvu na mamlaka, Kitambaa kiwe cha hariri inayongaa au velvet au kilicho tariziwa, Rangi iwe ya Dhahabu. Mavazi yaambatane na Vito vya dhahabu, Wanawake wapendelee kuvaa magauni ya kutokea usiku yawe ya dhahabu au rangi ya machungwa

MAGONJWA YA SIMBA:
Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama.Vilevile inatawala uti wa mgongo na mshipa mkubwa wa damu.Matatizo yao makubwa kiafya yanahusiana na maradhi ya kuumwa sehemu ya juu ya mgongo.Maradhi yanayotokana na damu kama shinikizo la damu la juu na chini na maradhi ya moyo.Vilevile wanaugua maradhi ya homa ya uti wa mgongo.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA SIMBA:
Wenye nyota hii wanatakiwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, machungwa, maboga, vitu vichachu kama ndimu au malimao na wapende sana kula nyama za ng'ombe, mbuzi na kondoo. Simba wanatakiwa wakaishi au watembelee nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Italia na Morocco na miji ni Bombay (India) na Roma (Italia)

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Simba ni Dhahabu. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni kama vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Simba ni Sandarusi unachoma siku ya Jumapili kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.
 
Hizo ni mbinu za shetani achana mambo nyota utakuja kutapeliwa na team assist ! At your own risk.
 
Haya mambo ya Nyota ni tofauti sana na Mimi.

Kuna watu ni wafuatiliaji wazuri sana, na wanavyo hadi Vitabu.

Nyota ni usanii tu, hamna lolote
 
Nyota ya kenge au mamba haipo? Nyota ya nyoka je ipo? Nyota ya mjusi au panya zikoje?

Mimi nina nyota ya Nguruwe unaweza kunipa utabiri? Niliwahi kusikia mtu akisema ana nyota ya mabiringanya, ndio ikoje hiyo shehe.
 
Nyota ya kenge au mamba haipo? Nyota ya nyoka je ipo? Nyota ya mjusi au panya zikoje?

Mimi nina nyota ya Nguruwe unaweza kunipa utabiri? Niliwahi kusikia mtu akisema ana nyota ya mabiringanya, ndio ikoje hiyo shehe.
Mbwahaaaaaa mbwahaaaaaa
 
Ila mm nahisi kanichana vilivyo maana 27/7 halafu 99%mule mule
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom