Maelezo ya Nyerere kwa Gen. Kombe na Membe kuhusu Jack Gotham

GARETHBALE

Member
Dec 22, 2013
76
332
MAELEKEZO YA MWL.NYERERE KWA JEN. KOMBE NA MEMBE KUHUSU JACK STEVEN GOTHAM.

Karibuni tena kuungana nami kati "series" na "episode" namba sita inayoelezea wasifu na historia ya mseminari, kachero, mwanasiasa, kiongozi na mwanadiplomasia Bernard Kamilius Membe.

Lakini kabla sijaendelea na "episode" niendelee kuwashukuru wasomaji wote wa jukwaa hili ambao bila kujali itikadi au utofauti wa uelewa lakini wananitia moyo wa kuandika bila kuchoka.Wakosoaji nao hawako nyuma lakini ndio raha ya maandishi.Lazima yapingwe ili kunogesha uandishi na kuboresha hoja.

Tuendelee....

Anajulikana kwa jina la Jack Steven Gotham.Maarufu kwa majina mawili Jack Gotham au JG.Siku za hivi karibuni vijana wengi wa mjini wamembatiza jina jipya,wanamwita "Burito".Jina la "Burito" linatokana na mtaa anaoishi kuamua kuupa hili jina kama njia yake katika kumuenzi Mwl.Julius Kambarage Nyerere. Huo mtaa unaitwa Burito Street.

Jack Steven Gotham ni chotara wa Kijerumani.Baba yake mzazi alikuwa rafiki mkubwa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Mama yake mzazi ni Mzanaki kutoka Butiama. Baba yake mzazi alifariki miaka mingi nyuma na kuzikwa mkoani Mbeya kwenye wilaya ya Mbarali.

Jack Steven Gotham sio jina geni kwenye familia ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere na kwa kiasi kikubwa maisha yake ya utoto hadi mwanzo wa ujana wake ameishi Ikulu na familia ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Hii ni kwasababu baada ya kifo cha baba yake alichukuliwa na Mwl. Julius Kambarage Nyerere na alimlea Ikulu wakati wa uongozi wake kama walivyolelewa kina Makongoro Julius Nyerere.Kwa lugha nyingine tunaweza kumtambua Jack Steven Gotham kama mmoja wa wanafamilia wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Mama yake mzazi na Jack Steven Gotham anaishi hapa jijini Dar es salaam.Nyumba yake ipo Magomeni wilaya ya Kinondoni. Jack Steven Gotham ni mtoto wa mwisho kuzaliwa kwa baba na mama yake.Lakini pia ana vinasaba vya undugu na mfanyabiashara maarufu Zacharia Hans Poppe kwa upande wa baba yake.

Jack Steven Gotham ni shabiki mkubwa wa timu ya mpira Simba Sports Club. Kuna wakati mmoja wa marafiki zake wa karibu aitwaye Salum Mpugusi aliwahi kunukuliwa kwamba Jack Steven Gotham kwenye miaka ya mwishoni mwa 1980s aliwahi kuidhamini timu ya Simba Sports Club kwa kuwapangishia nyumba maeneo ya Magomeni na kuwahudumia kwa chakula,usafiri na posho lakini hakuwahi kuruhusu suala hili litangazwe hadharani.

Jack Steven Gotham ana mke aitwaye Samira na wamebarikiwa kuwa na watoto watatu ambao ni Jesse,Joan na Jaffa.Jesse anasoma nchini Canada, Joan anasoma nchini Mauritus na Jaffa anasoma hapa nchini. Jack Steven Gotham ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa la St.Joseph la jijini Dar es salaam.

Ilikuwaje Jack Steven Gotham akajuana na Bernard Kamilius Membe na Jen.Imrani Kombe? Iko hivi:

Miaka miwili baada ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kustaafu pamoja na kuwa na wasaidizi kutoka serikalini aliamua kumwongeza Jack Steven Gotham katika orodha ya wasaidizi wake.Tofauti na wasaidizi waliokuwa wakilipwa na serikali yeye Jack Steven Gotham alikuwa msaidizi binafsi wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa akilipwa na Mwl. Julius Kambarage Nyerere kutoka katika fedha zake za mfukoni.

Pamoja na kwamba Mwl. Julius Kambarage Nyerere alimlea na kumsomesha Jack Steven Gotham kama mwanaye wa kumzaa lakini hakutaka kabisa kumtumikisha bila kumlipa chochote.Hii ni kwasababu aliamini Jack Steven Gotham bado ni kijana lakini pia ana majukumu ya kumsaidia mama yake mzazi na ndugu zake.

Hata baada ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere kustaafu na kuhamia nyumbani kwake Msasani bado Jack Steven Gotham alizoea kwenda kushinda na mara nyingine kulala pale.

Sasa ikatokea siku moja aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa "ofisi nyeti" kwa wakati ule Jen.Imrani Kombe na Bernard Kamilius Membe walienda nyumbani kwa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa shughuli ya kiofisi.

Wakati huo Bernard Kamilius Membe alikuwa anaongoza idara ya sekretarieti ndani ya "ofisi nyeti".Idara hii ndio uti wa mgongo wa shughuli za "ofisi nyeti".

Wakati Bernard Kamilius Membe akiongoza sekretarieti ya "ofisi nyeti" msaidizi wake alikuwa "Mchungaji" Dk.Modestus Kipilimba.Bernard Kamilius Membe ndiye ofisa wa "ofisi nyeti" mwenye historia ya kuongoza sekretarieti ya "ofisi nyeti" kwa miaka mingi zaidi kuliko mwingine yeyote akifuatiwa na "Mchungaji" Dk.Modestus Kipilimba.Bernard Kamilius Membe aliiongoza kwa miaka nane(8)wakati "Mchungaji" Dk.Modestus Kipilimba aliiongoza kwa miaka mitatu(3)tu.

Sasa basi baada ya Jen.Imrani Kombe na Bernard Kamilius Membe kuwasili nyumbani kwa Mwl. Julius Kambarage Nyerere walifanya kikao chao cha kiofisi na Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Walipomaliza wakati wanaaga na kuondoka ndipo Mwl.Julius Kambarage Nyerere alipowaomba wasubiri awatambulishe kwa mmoja wa vijana wake wanaomsaidia kazi zake binafsi. Ndipo akamwita Jack Steven Gotham.

Katika utambulisho wake Mwl.Julius Kambarage Nyerere alikuwa wazi kwa Jack Steven Gotham kuwa anaowaona mbele yake ni watumishi wa "ofisi nyeti" na kwamba angependa afanye nao kazi kwa karibu siku za mbeleni.

Kisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere akamwambia Jen.Imrani Kombe amwajiri Jack Steven Gotham au ikiwezekana kumtumia katika shughuli zao maalumu.

Akawajulisha kwa ufupi wasifu wa Jack Steven Gotham katika nyanja ya elimu huku akiwa kamsomesha nchini Cuba, Bulgaria, China na Algeria kupitia msaada wa rafiki zake.Na alijikita kwenye masuala ya teknolojia na elimu ya masuala ya kijeshi.

Baada ya utambulisho huo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere kuhusu Jack Steven Gotham kwa Jen. Imrani Kombe na Bernard Kamilius Membe ndipo Jen. Imrani Kombe akatoa maelekezo kwa Bernard Kamilius Membe kuchukua mawasiliano binafsi ya Jack Steven Gotham ili taratibu za kuchukua taarifa zake muhimu kabla ya kuajiriwa zianze.

Baada ya siku kadhaa Bernard Kamilius Membe aliwasiliana na Jack Steven Gotham na kuomba ampatie nakala ya vyeti vyake vya kuzaliwa pamoja na vya elimu yake pamoja na picha zake za pasipoti size.

Kuhusu taarifa zake nyingine muhimu hilo lilibaki kuwa ni suala la watu wa vetting wa "ofisi nyeti" ambalo hata yeye mwenyewe Jack Steven Gotham kwa wakati ule hakulijua kutokana na unyeti wa suala husika.

Baada ya miezi kadhaa kulitokea safari ya kikazi ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kwenda nchini Zambia.

Katika safari ile ilipaswa aambatane na Jen. Imrani Kombe pamoja na Bernard Kamilius Membe. Na kwakuwa wasaidizi wake wa kiserikali ni lazima waongozane naye basi "ofisi nyeti" kwa maagizo ya Jen. Imrani Kombe ikaorodesha jina la Jack Steven Gotham kuwa katika moja ya watu wao watakaoenda katika ile safari.

Ikampasa Jack Steven Gotham kuwasilisha hati yake ya kusafiria kwa Bernard Kamilius Membe ili "logistics" muhimu kwa ajili yake ziweze kuandaliwa.

Siku ilipowadia safari ikafanyika.Safari ikawa ya mafanikio. Moja ya majukumu waliyojipa Jen. Imrani Kombe na Bernard Kamilius Membe ni kuweka macho yao kwa Jack Steven Gotham namna anavyotekeleza majukumu waliyompatia kama anayafanya kama inavyopaswa.

Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema walikuwa wanampa test kama atawafaa. Sio Mwl. Julius Kambarage Nyerere,wasaidizi wake wa kiserikali au Jack Steven Gotham mwenyewe walijua kama pamoja na kwamba wapo Zambia kwa kazi ya kiserikali lakini kuna mmoja wao anafanyishwa mtihani wa majaribio bila yeye mwenyewe kujua.

Waliporejea Tanzania ikapendekezwa sasa Jack Steven Gotham ahudhurie kozi maalumu za masuala ya shughuli za "ofisi nyeti" na baada ya kuzihitimu ndipo alipoanza kuitumikia "ofisi nyeti" rasmi.

Kwahiyo Jen. Imrani Kombe na Bernard Kamilius Membe walitekeleza ombi la Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuhusu ajira ya Jack Steven Gotham kwenye "ofisi nyeti".

Baada ya kifo cha Jen. Imrani Kombe ndipo Jen.Apson Mwang'onda akachukua nafasi kama Mkurugenzi Mkuu wa "ofisi nyeti".

Ni miaka hiyo hiyo ambayo pia Bernard Kamilius Membe alikuwa kahamishiwa kikazi nchini Canada kwenye ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo basi Jack Steven Gotham akabaki nchini Tanzania akiendelea na majukumu mengine hadi pale "ofisi nyeti" ilipompendekeza kuwa Mshauri wa masuala ya usalama nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo chini yake aliyekuwa Rais marehemu Laurent Desire' Kabila.

Baada ya kifo cha rais Laurent Desire' Kabila,Jack Steven Gotham alirejeshwa nchini na kuwa benchi akisubiri kupatiwa jukumu lingine na "ofisi nyeti".

Lakini kama mjuavyo hakuna binadamu asiyepitia changamoto katika maisha yake.Mwaka 2000 inasemekana kulitokea hali ya kutoelewana kati yake Jack Steven Gotham na Jen. Apson Mwang'onda hadi kupelekea moja ya magazeti ya serikali kutoa taarifa kwa umma kuwa Jack Steven Gotham sio mtumishi tena wa "ofisi nyeti".

Taarifa ile ikaenda mbali zaidi na kutamka kwamba Jack Steven Gotham hajawahi kuwa mtumishi wao kabisa.Hii tayari ikawa ni sintofahamu kubwa. Nadhani mwandishi wa taarifa ile alijikanganya.

Swali la kujiuliza ikawa ni nani wa kumsafisha Jack Steven Gotham? Je Jack Steven Gotham aongee na vyombo vya habari kukanusha taarifa ile?

Jibu ikawa sio sahihi yeye kuzungumza na vyombo vya habari.Hapa ndipo Bernard Kamilius Membe alipoamua kujipa jukumu la kumsaidia Jack Steven Gotham.

Na ndiye mtu pekee aliyekuwa kabaki maana Jen. Imrani Kombe alikuwa katangulia mbele ya haki.

Na wakati huo Bernard Kamilius Membe alikuwa karejea nchini kutoka Canada alipokuwa anafanya kazi katika ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ndio kwanza alikuwa hana hata mwaka mmoja tangu awe mbunge wa jimbo la Mtama.Bernard Kamilius Membe alipata nakala ya lile gazeti.

Akalisoma na kuamua kwenda kuonana na Jen. Apson Mwang'onda. Walichozungumza imebaki kuwa siri baina yao (Bernard Kamilius Membe na Jen. Apson Mwang'onda) na hadi umauti unamfika (Jen.Apson Mwang'onda) hakuna yeyote baina yao aliyewahi kusema kwa mtu mwingine ni nini walichozungumza kuhusu suala la Jack Steven Gotham.

Ila tu mafanikio ya maongezi yao (kikao chao) yalionekana kwani lile gazeti lilitoa taarifa ya kukanusha taarifa ya mwanzo waliyochapisha kuhusu Jack Steven Gotham.

Hivyo ndivyo Jack Steven Gotham alivyosafishika. Na hivi ndivyo Jack Steven Gotham na Bernard Kamilius Membe walivyokutana na kufahamiana.

"Episode" ijayo nitaelezea undugu wa hiari kati ya Bernard Kamilius Membe na mwanasiasa wa upinzani Sam Ruhuza.

Tukutane tena kesho muda kama huu.
 
Taifa hili nizaid ya ulijuwavyo. Wanaishi kwakulana na wakimaliza wanafuta midomo nakuja kula mboga za majani. Tukutane 2020 kwa neema za Mungu
 
Mkuu.

Masahihisho kidogo.

2. Imrani Kombe hakuwa Generali (4 Stars), Alikuwa Luteni Generali (Liutenant General, 3 Stars )

2. Apson Mwang'onda hakuwa Jenerali

Ni katika kuweka ladha ya uzi.
Twende kazi

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
mleta thread unamvimbisha Membe Bichwaa...

atambue NEC ya Joni sio ya mchezo mchezo,atanyonyolewa..ooohh!

yy atulize boli

"right place at right time,i will strikes.!!" Paul Kagame akimtaarifu Mkwere



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nzuri sana hii! endelea za kushusha nondo/ubuyu, pia mwambie membe tunamtakia kila lililo jema kwenye mahojiano yake na kamati ya usalama na maadili ya chama chake.
 
Taifa hili nizaid ya ulijuwavyo. Wanaishi kwakulana na wakimaliza wanafuta midomo nakuja kula mboga za majani. Tukutane 2020 kwa neema za Mungu
Maanake Imran kombe na Apson wameliwa vichwa?je kipilimba atapona?wewe je haupo kwenye series ya kuliwa vichwa?au Membe nae analiwa kichwa?Okh na mimi naisubiri 2020 kwa hamu sana!!!ngoja tuone misuli ya TISS kati ya waliotoswa kwenye mfumo na waliowekwa kwenye mfumo!!!
 
Mkuu Garethbale uwe na ahadi za kizungu!nimeusubiri huu uzi kwa hamu sana hadi nikafikiri MODS WANAKUHUJUMU COZ WANAOGOPA KESI ZA KUBAMBIKIWA!!!
 
Back
Top Bottom