hakuna shida
Member
- Dec 16, 2015
- 25
- 5
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
MAELEZO KUHUSU MRADI WA UMEME MBOPO TEGETA
DAR ES SALAAM
Februari 2, 2016 kwenye blogi ya Michuzi kuna mteja wetu kutoka Wilaya ya Kitanesco Tegeta alilamikia Shirika kuchelewesha Mradi wa kupeleka umeme eneo la Mbopo.
UKWELI NI KWAMBA: Mradi wa kupeleka umeme Mbopo unagharama ya Tsh.236,396,581.73, na umegarimiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa asilimia 100.
UKUBWA WA MRADI: Mradi wa kupeleka umeme Mbopo unagharama ya Tsh.236,396,581.73, na unagharamiwa na Shirika la umeme Tanzania kwa ailimia 100. Mradi unahusisha;
1. Ujenzi wa laini ya msongo wa kilovolti 33 yenye urefu wa kilomita 8 na nguzo 93
2. Transfoma kubwa ya kusambaza umeme (100kva 33/0.4/0.23kv-01)
3. Nguzo 62 za umeme wa msongo mdogo ya njia tatu yenye urefu wa kilomita 3.
KAZI ILIYOFANYIKA MPAKA SASA:
1. Nguzo zote 93 zimeshasimamishwa
2. Waya zimevutwa kwa urefu wa kilomita 2 kutoka Mbopo zahanati hadi Pangaboy Bar.
SABABU ZA KUCHELEWA KWA MRADI:
1. Mradi huu umechelewa kukamilika kutokana utaratibu wa manunuzi ya baadhi ya vifaa vya ujenzi kwenye mradi.
2. Kukosekana kwa Njia ya kupitisha umeme (way leave) wakati wa zoezi la kusimamisha nguzo lilipoanza.
AHADI KWA WANANCHI:
Baada ya kupatikana kwa vifaa hivyo, Shirika linategemea kuanza tena utekelezaji wa Mradi huu Jumatatu Februari 08, 2016 na kukamilika Februari 26, 2016.
MIRADI MINGINE MUHIMU:
Pamoja na mradi huu, mkoa pia una miradi ambayo linategemea kujengwa kwa mwaka huu 2016. Taratibu za kuwapata wankandarasi zinaendelea.
1. Mradi wa kupeleka umeme Block 8 Mbweni Mpiji,
2. Mradi wa kupeleka umeme Block 7 Mbeni Mpiji,
3. Mradi wa kupelekea umeme Mbweni Teta,
4. Mradi wa umeme Mabwe pande Kikwete Vision,
5. Mradi wa kupeleka Umeme Kisauke
Uongozi unaendelea kusisitiza kwa wateja wake kuwa Mipango mizuri na inayotekelezeka ya kuwapatia watanzania umeme wa uhakika ipo na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu