Madudu ya shule za Michepuo wa Kiingereza

Madudu ya shule za Michepuo wa Kiingereza

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,729
Naungana na mwandishi wa Gazeti la Mwananchi la leo Jumanne Septemba 19, 2017 kuhusu kichwa cha mada hapo juu, kusikitika kwa yanayojiri kwenye hizo shule.

Gazeti hilo limekariri matokeo ya operesheni iliyofanyika katika Manispaa ya Ilala, jiji la DSM kukagua shule zenye mchepuo wa kiingereza (English medium schools) na kugundua madudu yafuatayo:

1) baadhi ya shule hizo hazina usajiri

2) shule zina mazingira duni na hatarishi kwa afya za watoto (ona picha ya godoro la shuleni), ati watoto wanarundikwa na kulazwa kwenye vyumba vidogo visivyo na madirisha ya kuingiza hewa ya kutosha.
8b8c8e9bf0a3f07d3694eb459f7da97a.jpg

3) shule kama ya Gefan, inasemekana, pamoja na kuwa na wafunzi 92, haina hata darasa moja kasoro vyumba vidogo vyenye joto kali ndani.

Iwapo hali kama hiyo ipo, mbali na kutoa elimu duni, wakisisitiza kujua kusoma na kuongea kiingereza, basi kuna haja ya Serikali za Mitaa kuanzisha kampeni ya kuhakiki shule zote za michepuo ya kiingereza.

Tunapozungumzia elimu bora ni pamoja na mazingira ya kutolea hiyo elimu. Na hili lisiwe tu kwa shule za umma.
 
Shule zote, licha ya kuwa na madarasa ya kutosha, waalimu wenye sifa husika, lazima ziwr na viwanda cha michezo kwa ajili ya wanafunzi wao. Shile zimejibana au zina maghorofa, hawajali afya na ukakamavu wa kushiriki michezo mbalimbali.
 
hapo naungana na ninyi kingne shule hizi hawatakagi wanafunzi wafeli ht mitihan ya ndani mtoto atapata alama nyingi wakat hamna kitu kichwan ili mzaz ufurai ulipe karo
 
Back
Top Bottom