Madudu ya CCM haya hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madudu ya CCM haya hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibajaj, Jul 22, 2011.

 1. k

  kibajaj Senior Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha mapindizi kimeendelea kufanya yale wengi wanayoyaona kama madudu na kubebana, hii imeonekana zaidi baada ya katibu mkuu jana kumpa likizo tena yenye malipo katibu mkuu wa nishati na madin bilia kuonyesha kwa dhati kuwa jambo hili ni la aibu na wizi. Na baadaya amesema kuwa anapisha uchunguzi kwani ni tuhuma tu ambazo haziaminiki wakati barua ya madudu yake ipo na imeanikwa hadi kwenye magazeti. Sijui hii serikali ilitaka ushahidi kutoka kwa malaika ndo iamin au nyerere afufuke ndo waamaini.

  Mbaya zaidi ni pale wabunge walipopingwa marufuku kulijadili jambo hili ili kupisha vyombo husika vifanye kazi yake na kama kawaida ya watanzania mtu huyu atakutwa hana hatia. Na mbona Dowansi iliuzwa sualaa likiwa bado mahakamani?
  Ya ricmond na lowassa yaliwacost sana kwenye uchaguzi wa 2010 sasa haya yatawanyima uongozi na waanze kukimbia mapema maana watashtakiwa kwa uzembe na kufungwa.
   
 2. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwisho wa CCM huo waja
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mimi haya mambo ya hawa watu nimeisha ya2hoka, wanafanya madudu mengi. Kukisafisha chama namwachia kazi katibu mukama!
   
 4. MWAGONA

  MWAGONA Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ya kweli mwisho wa kila kitu huwa na una vituko vyake au kwa upande mwingine ni ''features of fall of ccm '' migomo isyo kauka,kuanguka kwa thamani ya tshilingi,mgao wa umeme usio isha,mafisadi wa kila aina,mikataba zaidi ya mibovu kuuwa wananchi wasio na hatia,kufunga vyuo kila wakati,maisha mabovu zaidi,hali mbaya saidi na kuchukiwa kwa serikali kwa kila pande ya tanzania.mwishooo umefika mtaniambia
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  ukiona hivyo ujue mkuu anahusika na ule mlungula,..
   
 6. Salas

  Salas JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Rais kikwete anasalitiwa na watendaji wake:
  Zaidi ya asilimia 50% ya watu waishio vijijini hawana huduma ya maji, ikiwa asilimia 8O% ya watanzania ndio inakadiriwa kuwa wanaishi maeneo ya vijijini. Kwa mujibu tafiti zilizofanywa na wizara ya afya na asasi nyingine zinaonyesha kuwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano ni 20,000 kwa mwaka ikiwa ni sawa na mabasi 333 yanayopata ajali kila mwaka pasipo kuwa na mtu aliyesalimika kwenye ajali. Machache kama sio hakuna yamefanywa kufikia asilimia hii ya watu wanaokosa huduma hii muhimu.

  Tumeshuhudia wabunge wakiwa kidedea kusiamamia swala la umeme katika bunge lakini nguvu hizo pia zingeelekezwa kwenye sekta ya maji zingezaa matunda ambayo yangepunguza gharama kubwa inayotumika na wizara ya afya katika ununuzi wa madawa ya magonjwa yanasababishwa na ukosefu wa maji au matumizi ya maji machafu na athari kadha wa kadha katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kupoteza nguvu kazi.

  Katikahali ya kukangaynya ikiwa ni muendelezo wa usaliti kwa muheshimiwa rais wetu ni ile hali ya Tanzania kukataa kupiga kura ili kutambua swala maji kama haki ya binadamu katika uchaguzi wa umoja wa kimataifa kutambua haki Maji uliofanyika tarehe 28 july 2010. Tanzania ikiwa nimiongoni mwa nchi 41 zilizopiga kura ya absentation ikiwa ni kuficha aibu ya kukataa haki hii istambulike ikiwa imeongozwa kidedea na USA na nchi nyingine na za ulaya na makoloni ya ulaya ikiwemo kenya. Licha ya hayo nchi 122 zilipiga kura ya kutambua haki hii right to water and sanitation.

  Katika Muendelezo huu wa aibu, ukiwa unafanywa kwa lengo ama la kumdhalilisha Mheshimiwa rais au kutowajibika kwa viongozi wa idara husika Mheshimiwa rais alishapitisha sheria ya maji na usafi wa mazingira sheria namba 12 ya mwaka 2009 inayotambua kuwa maji ni haki ya binadamu. Nita quote " 4.-(1) The objective of this act is to promote and ensure the right of every person in Tanzania to have access to efficient, effective and sustainable water supply and sanitation services for all purpose"

  Nachelea kudadavua kuwa huu ni usaliti wa makusudi ambao pia umewahi kufanywa katika kipindi cha vijiji vya ujamaa ambapo jitahada safi za Mwalimu Julius Kambarage nyerere zilipotoshwa na walarushwa wachache katika kuhujumu mawazo sahihi ya Mwalimu ili kuweza kufikisha huduma za jamii kwa watu wake ikiwemo maji na nyinginezo. Tukumbuke pia mwalimu aliweza kufanya kazi katika miongo miwili kwa kauli mbiu ya maji kwa wote. Swali ni Je kwanini hawakusaini in favor ya right to water and sanitation na wakati sheria ziko wazi ??????

  Hizi ni hujuma kama zile zinazoendelea kwenye miradi ya vijiji kumi ambapo japo wizara husika haitaki kuweka bayana kuwa vijiji sio kumi tena ila vitatu kutokana na ubadhirifu wa wataalamu washauri ambao mashirika yameundwa kiuhuni ili kuhujumu nia safi ya Rais kuwapatia huduma ya maji watu wake. Gharama za mradi zimekuwa kubwa kushinda fedha na waziri mwenye dhamana anakiri hilo kwenye hotuba yake ya wiki ya maji ili hali anajua anajua kuwa sio mapendekezo ya wananchi yaliyopitishwa kwenye design ya hiyo miradi ni wizi wa wataalam washauri ili makampuni ya kijanja ya ujenzi yaje kukwapua hizo hela. Huu ni ufisadi mwingine kwa ajili ya kuja kumchafua mheshimiwa rais.

  Ninasisitiza kuna haja ya kila mtu kusimama kwenye nafasi yake katika kuleta maendeleo ya hii nchi, maisha bora yatafikiwa pale tu kila mtu mmoja mmoja atakapofanya kazi kikamilifu katika nafasi yake.

  hakika kikulacho kinguoni mwako huu ni muendelezo wa usaliti dhidi ya rais wetu Mtukufu wa Jamuhuri ya Tanzania. ​
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ukisema zaidi ya asilimia 50% ya population ya vijijini haina maji bado utakuwa umependelea sana. Sema zaidi ya asilimia 90. Vinginevyo kama unasema yale maji ya kufukua chini. Maana mjini kwenyewe ni 13% tu ya population yote ndiyo inapata maji safi ya bomba. Na vijijini ni 1% tu ya population ya nchi nzima ndiyo inapata maji safi ya bomba.
  Na hiyo mortality rate ya watoto 20,000 kwa mwaka sina uhakika nayo. Fuatilia vizuri data mkuu, idadi tu ya wanawake wanaokufa kwa mwaka kutokana na matatizo ya uzazi inazidi laki moja halafu watoto wanaokufa kwa mwaka wawe 20,000 tu, sina uhakika.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Eh! Ngoja niliangalie boriti la jicho langu kabla sijacomment!
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Kama huna uhakika kwa nini umemwaga pumba hapa, siunggenda kwanz akutafuta mchele (uhakika) halafu ndio urudi kumwaga vitu vya uhakika? Unanchekesha!
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tumekuzoea! Huwa unafikiria kwa kutumia makalio, kwani nani asiyekujua. Badala ya kusubiri nikutafunie kila kitu shika kopi hii hapa usome halafu utuambie wewe pumba zako ni zipi?
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Ama we kweli unashangaza, hebu soma hiyo report uliyoiweka ukurasa wa 4 halafu sema hapa ni nini hicho? Tazama kabla ya kuchukuwa nchi Kikwete tulikuwa wapi na baada ya kuchukuwa kaipeleka wapi? Utaona haya nakwambia na wala hautorudi kujibu hoja hii, nna uhakika.
   
 12. L

  Lua JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  inasikitisha sana, kama mtuhumiwa wa ufisadi anapewa likizo na malipo wakati kuna watumishi wanaodai fedha za likizo hadi leo hawajalipwa, hivi tunaelekea wapi?
   
 13. s

  sanjo JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  A corrupt system will always strive to maintain the status quo by discouraging taking responsibility and accountability.
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Yaani wewe unanielekeza nisome ilhali mimi ndo niliyeandika? Au mimi ndo nikuelekeze wewe? Kwa hiyo pumba ulizosema mimi nimeandika ni zipi? Katika kusoma hiyo report umeona mortality rate ya watoto chini ya miaka mitano ni 20,000 kwa mwaka? Sijadili habari ya hali ilikuwaje huko nyuma na ilivyo sasa? Soma vizuri post yangu ya msingi utaelewa ni nini nilichokuwa nimebishia mimi. Hatubishani juu ya kuongezeka au kupungua, bali ni kwamba wanaokufa ni zaidi ya 20,000. Sawa?
   
 15. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maisha hoi kwa wasio nacho maisha bora kwa kila fisadi.
   
 16. m

  mwl JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 180
  Wachekesha wachekesha masikini hujijui, bure wajihangaisha hakutaki JK. Hivi inahitaji mwenye macho aeleze alipotufikisha Jk? Wenye ulemavu wa macho pia wanalalama.
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  CCM ni bomu linalosubiriwa kupasuka!!!!
   
 18. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Nachoshangaa mimi hadi sasa si polisi wala TAKUKURU waliomuhoji. CDM ebu saidieni Tifa kumuuliza IGP Mwema au Hosea wanasubiri nini japo kumuhoji huyu Jamaa.
   
Loading...