Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Laissez faire ni neno la kingereza ambalo kwa tafsiri yangu isiyo rasmi linamaanisha ile tabia ya kuyaachia mambo yajiendee tu, kiwepesi wepesi tu, kirafiki pasipo kujali nani anayeumia na kwa kiwango gani.
Awamu ya nne ilitawaliwa na Laissez faire, mambo ya msingi yakachukuliwa poa tu, na yale ambayo ni poa tu yakaonekana ndio ya maana kwa jamii. Wakati watu wapo kwenye matatizo makubwa, wale waliotakiwa kuonyesha kuguswa wala hawakujali, ndio kwanza walikuwa wanabembea kwenye zile bembea za umeme, nje ya bara la Afrika. Mambo kama yale ya yule mama kujifungua huku akikosa msaada kule butimba mwanza, kama ingekuwa ni enzi zile, yangeundiwa tume, halafu baada ya siku nyingi kupita, ndio ingekuwa imetoka hiyo. Lakini awamu ya tano imelishambulia tatizo tena haraka sana.
Awamu ya tano imekuja tofauti kabisa yale ambayo siku za nyuma yalichukuliwa kama vile ni madogo kama ile rushwa ya kule ligula Mtwara, sasa hivi ni mambo makubwa kiasi cha waziri mkuu kuingilia kati. Hakuna Laissez Faire katika awamu hii, mnyonge anatetewa ipasavyo. Lakini mnyonge huyo huyo anao wajibu wa kutambua kile kinachopaswa kuwa mchango wake kwa maendeleo ya Taifa. Serikali inapotimiza wajibu wake na raia anaachiwa jukumu la kutimiza wajibu wake, na sio kuishia kulalama kila kukicha.
Laissez Faire iliumiza wengi sana, wale wale maafisa wa serikali waliowapita watu wakiwa wamepanga foleni huku wao wakipiga miluzi, sasa hivi wanawakimbilia wale wale waliowaona kama vile vikatuni. Natumaini ni nguvu ya gongo ambayo imehifadhiwa kwenye chupa ya soda.