Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Madiwani wa CHADEMA na CCM wameungana na kumng'oa madarakani mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kwa madai kuwa amekuwa akitumia madaraka yake vibaya, na kushindwa kuendesha vikao vya baraza kwa kufuata kanuni na taratibu.
Katika hali isio ya kawaida , mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Dr. Hunter Mwakifuna alipotaka kufungua kikao cha baraza la madiwani hao wakaungana pamoja kutoka chama pinzani cha CHADEMA na chama tawala cha Mapinduzi CCM na kususia kumsikiliza, huku wakiimba wimbo na kupiga makofi mezani pasipo kukoma.
Baada ya kukosekana maelewano katika kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kyela akasimamisha kikao kwa muda na kurejea baada ya dakika 15, ambapo wajumbe waalikwa walitolewa nje kupisha maamuzi ya kamati ya ulinzi na usalama , hata hivyo haikuzaa matunda hadi kikao kilipoahirishwa mpaka kitakapopangwa upya.
Kwa mjibu wa madiwani hao, mwenyekiti anadaiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za miradi mbalimbali zikiwemo million 211, kushindwa kuendesha vikao kinyume na utaratibu, kutumia madaraka yake vibaya na kuwalinda viongozi wanaotuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha.
Waandishi wa habari walipomhoji mwenyekiti Dr. Hunter kuhusu tuhuma hizo amesema kuwa hazina ukweli kwa kuwa tume za uchunguzi wa madai hayo zilizoundwa zimebaini fedha kwa baadhi ya miradi zimepatiwa majibu na kwamba tuhuma zingine bado zinachunguzwa kwa kufuata sheria.