Madiwani Chadema, CCM wasusia kikao

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
MADIWANI kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Mamlaka ya Mji wa Tarime pamoja na Diwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bomani, Godfrey Masub wamesusia kikao cha Baraza la Mamlaka hiyo kilichofanyika leo. Wamesusia kikao hicho kwa kile walichosema ni kutaka watumishi wanaodaiwa kwa namna moja ama nyingine kuhujumu mamlaka hiyo waondolewe.

Kikao kilifanyika jana chini ya uenyekiti wa Mwita Mantago na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri, Amos Sagara.

Mkuu wa Wilaya, Henjewele mbali na kuwatahadharisha wajumbe hao kutotoka nje kwa kuwataka malalamiko yao wayatolee katika kikao hicho na kupata majibu, wajumbe hao waliondoka wakidai hawawezi kukubali kuburuzwa na Mwenyekiti wa Baraza , Mantago. Wengine waliohudhuria ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Silvanus Gwiboha, Katibu Tawala wa Wilaya, Ernest Kabohola na Katibu Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Hashimu Barongo.

Kiongozi wa kambi ya upinzani kupitia Chadema, Christopher Chomete ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sabasaba pamoja na wenzake, walihoji kwa nyakati tofauti sababu za kutoondolewa baadhi ya watumishi kwenye Mamlaka ambao kikao cha Kamati ya Uchumi na Fedha kiliazimia wachukuliwe hatua hiyo kwa madai kuwa ni wabadhirifu.

Wengine waliotaka waelezwe sababu za hatua hiyo kutochukuliwa dhidi ya watumishi hao, ni Diwani wa Kata ya Nyamisangura, Thobias Ghati (Chadema) na Diwani wa Kata ya Bomani, Godfrrey Masubo (CCM). Wajumbe hao waliwataja baadhi ya Watumishi ambao walidai wanapaswa kuondolewa ni pamoja na Mkuu wa Soko la Tarime mjini, Balthazal Leos, Mweka Hazina wa Mamlaka, Christina John na Mkuu wa Soko la Rebu, Meshark Matiko.

Wanapinga pia mfanyabiashara, Mwita Urembo kutoza ushuru katika maduka mbalimbali na kuchukua asilimia 20 ya mapato. Wanadai mfanyabiashara huyo hutoza wastani wa Sh 2,841,000 na huchukua asilimia 20. Wakati huohuo, madiwani hao wanadai upo ufisadi katika upangishaji wa majengo ya Mamlaka. Wanadai yanapangishwa kwa gharama za chini ikilinganishwa na thamani yake. Awali Ofisa Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Hashimu Barongo alidai kuwa Mamlaka hiyo katika kipindi cha Julai 2010 hadi Machi mwaka huu ilikusanya Sh 135,640 ,100 na imetumia Sh 135,031,985.

HabariLeo
 
Madiwani wanatakiwa wawe hivi, sio pale ubadhirifu unapofanyika wanakaa kimya!
 
Awali Ofisa Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Hashimu Barongo alidai kuwa Mamlaka hiyo katika kipindi cha Julai 2010 hadi Machi mwaka huu ilikusanya Sh 135,640 ,100 na imetumia Sh 135,031,985.

HabariLeo


Duh!..haya mapato na matumizi hesabu zake ni kiboko!
 
Wasiishie kutoka kwenye vikao. Wanatakiwa waje kwetu na kutueleza sababu za kutoka kwao. Tena watumie mikutano ya hadhara kwenye kila kata ili iwafikie wananchi waliowachagua moja kwa moja na sio kupitia magazeti (tena habari leo!?). Hiyo ndio dawa ya hao mafisadi. Naomba na diwani wangu, Mh. Ephata Nanyaro uchukue ushauri wangu huu!
 
Back
Top Bottom